Dar Es Salaam
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendesha mafunzo ya namna
ya kuwasilisha madai kupitia mifumo ya TEHAMA kwa maafisa wa Dawati la Mafao wa
Jeshi la Polisi Tanzania.
Akizungumza
na maafisa hao jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul-Razaq
Badru, amesema, kwa sasa PSSSF imejikita katika kutoa huduma zake kwa njia ya
TEHAMA ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama na wadau.
“Kisheria
tumepewa jukumu la kusimamia masuala ya pensheni kwa watumishi wa umma na Jeshi
la Polisi ni moja kati ya makundi maalum yanayohudumiwa na PSSSF. Kwa kutumia
huduma zetu za kidijitali, tunajitahidi kutoa huduma sahihi na kurahisisha mnyororo
wa utoaji huduma.”
Akieleza
jinsi PSSSF inavyokwenda na usasa, Bw. Badru alibainisha kuwa PSSSF imeanzisha huduma
mbalimbali za mifumo ya kidijitali ikiwemo PSSSF Kiganjani, ambapo mwanachama
anaweza kujihudumia mwenyewe ikiwa ni pamoja na wastaafu kujihakiki kupitia
simu janja mahali popote bila ya uhitaji wa kufika kwenye ofisi za PSSSF.
Naye
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Mbarouk Magawa, alisema Mafunzo kwa maafisa wa
Polisi yanakusudia kuleta ufanisi na uwazi katika kudai mafao kupitia njia za
kidijitali.
“Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha wanachama wanapokea mafao
yao kwa wakati na kwa ufanisi.” Alisisitiza.
Awali
Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, CP Suzan Kaganda, akizungumza kwa niaba
ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillius Wambura, alisema hatua hiyo ni
muendelezo wa utekelezaji kwa vitendo wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyotoa Septemba 2024, wakati wa
Mkutano Mkuu wa Makamanda na Wakuu wa Vikosi wa Jeshi la Polisi, kuhusu
matumizi ya TEHAMA kwenye Utendaji wa Jeshi hilo.
CP
Kaganda amewahimiza maafisa hao kutumia fursa hii ya kipekee, kuwa wepesi
kujifunza ili waweze kwenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.
“Mfumo
wa kuwasilisha madai kupitia mtandao utasaidia wanachama kufuatilia madai yao wenyewe kwa
haraka na kwa uwazi.” Alisisitiza.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul-Razaq Badru, akizungumza na makamanda hao wa Jeshi la Polisi
Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, CP Suzan Kaganda
Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, CP Suzan Kaganda
Mkurugenzi wa Uendeshaji, PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) G.A Semiono
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), David Misiime
Baadhi ya Makamanda na Maafisa wa PSSSF
Baadhi ya Makamanda na Maafisa wa polisi wakiwa kwenye kikao hicho
Baadhi ya Makamanda na Maafisa wa polisi wakiwa kwenye kikao hicho
Mkurugenzi
Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul-Razaq Badru (kulia) na maafisa wengine wakiongozana na
mgeni rasmi, Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, Jeshi la
Polisi, CP Suzan Kaganda mara baada ya kufungua kikao hicho jijini Dar es
Salaam Mei 14, 2024.