Mhe. Dkt. Tulia Ackson, aongoza kikao cha kuratibu Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewasili Ofisini kwake Geneva nchini Uswisi leo tarehe 15 Mei, 2024 na kuongoza kikao cha utangulizi cha maandalizi ya kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani kinachotarajiwa kufanyika tarehe 16 na 17 Mei, 2024 nchini humo.

Kikao hicho kinatarajiwa kuhusisha Maspika Wawakilishi kutoka Mabunge ya Kanda 6 za Kisiasa na Kijiographia, Wajumbe wa Kamati ya Uongozi na Uongozi wa Majukwaa na Umoja kwa ujumla wake.

Aidha, Mkutano huo wa Maspika Duniani utakaofanyika mwaka 2025 utaangazia kuweka ajenda za kuchakata changamoto zinazoendelea kuikumba Dunia.

Related Posts