Matumizi ya nishati chafu yanauwa Watanzania 32,000 kila mwaka

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Seleman Jafo amesema takwimu zinaonesha takribani ya Watanzania 32,000 kila mwaka wanapoteza maisha kwa sababu hawatumii nishati safi.

Akizungumza leo Mei 17, 2024 na Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika Paris nchini Ufaransa Mei 14, mwaka huu ambapo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alikuwa Kinara na Mwenyekiti Mwenza katika mkutano huo wa Kimataifa.

Dk. Jafo amebainisha kuwa: “Afrika sasa watu milioni 900 wanahangaika na nishati safi ya kupikia na takwimu zinaonyesha sisi Tanzaniani takribani 32000 kila mwaka wanapoteza maisha kutona na matumizi ya nishati isiyokuwa salama kupikia,” amesema.

Amesema mkutano uliofanyika Paris nchini Ufaransa hamasa yake kubwa imetoka Tanzania ambaye Rais Dk. Samia katika mkutano wa mwaka jana wa Mabadiliko ya Tabianchi ilikuwa chanzo kikubwa cha kuchagiza mkutano huo Rais amewaheshimisha kwa sababu wote waliokuja pale ajenda ilikuwa ya Tanzania.

Dk. Jafo amesema hekta laki 46,942 ni uharibifu wa mazingira kila mwaka hiyo ni changamoto kubwa na kwamba ili kuondokana na changamoto hiyo lazima wahakikishe kupunguza uharibifu wa mazingira kuondoka huku na kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia.

“Ili kutimiza malengo kufikia mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia lazima wapate elimu ni muhimu kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya nishati safi,” amesema Dk. Jafo.

Akizungumza Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Wizara inaendelea kutekeleza agizo la Rais Dk. Samia la kuleta pamoja wadau na wabunifu ili kusaidia Watanzania kutumia gesi ya kupikia kwa kulipia kuanzia shilingi elfu moja hadi 10,000 na kuendelea kulingana na matumizi yake kama ilivyo kwenye luku za umeme.

Amesema umuhimu wa wananchi kutumia nishati safi ya kupikia kwaajili ya kuepuka kuhatarisha uharibifu wa mazingira ndani ya nchi na nje kwa ujumla.

“Kuboresha teknolojia mbalimbali za nishati safi ya kupikia kwa sababu siyo LPG peke yake au gesi peke yake zipo teknolojia nyingi tukitaka kupunguza gharama ni lazima kuwekeza kwenye bunifu mbalimbali,”amesema Kapinga.

Amefafanua kuwa wanaendelea kuboresha miundombinu ya umeme ili Watanzania wengi wakipata umeme wa uhakika watumie majiko ya umeme yaliyoboreshwa amba mtumiaji wa pressure cooker uatatumia chini ya unit moja kupika maharage kwa muda mfupi.

“Tunaendelea kuhamasisha tuwe wabunifu wa teknolojia nyingine za nishati safi ya kupikia ili kupunguza gharama, wapo wadau tumeanza kuwaleta pamoja ili kuhakikisha tuna teknolojia nzuri mfano M Gas wao wanateknolojia yao unaweza kununua gesi kiasa chochote unataka kuanzia elfu 1,000, 2,000 au 5,000 na hili inawezekana,” amesema Kapinga.

Ameongeza kuwa elimu bado inahitajika mfano Dar es Salaam ni mjini lakini wanaongoza kwa matumizi ya mkaa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus amesema malengo ya mkutano huo kuipa kipaumbele nishati safi ya kupikia anga za kimataifa japo lilikuwa linahusisha nchi za Afrika.

Amesema ajenda za mkutano huo ni paomoja kuwepo na sera kwasababu nchi nyingi hazina sera ya nishati safi ya kupikia na walikuwa kushawishi kuwepo na sera nchi mbalimbali na kuharakisha ushirikiano wa wadau mbalimbali.

“Taasisi ya Nishati ya Kimataifa (IIE) inakadiriwa kuwa na uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 4 zitahitajika kila mwaka barani Afrika ili wote waweze kuwa na nishati safi ya kupikia ifikapo 2030,”amesema Zuhura.

Related Posts