Rais Mwinyi alitoa pongezi hizo wakati akifungua semina ya uwekezaji na elimu ya fedha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanahisa wake na Watanzania kuelekea Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa utakaofanyika Jumamosi Mei 18, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Alisema kuwa Benki ya CRDB imeendelea kudhihirisha kivitendo kuwa “Benki kiongozi” nchini kwani kila mwaka imekuwa ikiendelea kutoa faida ya uwekezaji kwa wanahisa wake huku akizitaka taasisi nyengine za umma na binafsi kuiga mfano.
“Nimefurahishwa pia kusikia mwaka huu Bodi ya Wakurugenzi imekuja na pendekezo la ongezeko la asilimia 11 ya gawio kwa hisa. Wanahisa wa Benki ya CRDB mnastahili kutembea kifua mbele kwa ongezeko hili,” aliongezea Rais Mwinyi.
“Niwapongeze Benki ya CRDB kwa kuongoza katika utoaji wa elimu ya masuala ya fedha kwa Watanzania. Siku chache zilizopita, mliandaa semina mliyoiita CRDB Bank Uwekezaji Day, mimi niliifuatilia kupitia televisheni,” Rais Mwinyi alisema huku akiitaka benki hiyo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza ujumuishi wa kifedha.
Katika hotuba yake, Rais Mwinyi pia alisisitiza umuhimu wa sekta ya fedha katika maendeleo ya taifa, akitambua mchango mkubwa wa Benki ya CRDB katika kuimarisha uchumi wa Tanzania, bara na Zanzibar. Alieleza jinsi Benki ya CRDB imekuwa mshirika muhimu katika kuendeleza dhana ya Uchumi wa Buluu, kupitia programu kama vile ‘INUKA na Uchumi wa Buluu’, ambazo zimechangia sana katika sekta za utalii, kilimo, ufugaji, uvuvi, mafuta, biashara, na ujasiriamali.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni mwanahisa wa Benki hiyo kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF). Dkt. Laay amewakaribisha Watanzania wengine kuwekeza ndani ya Benki ya CRDB ili nawao waanze kunufaika na gawio nono ambalo limekuwa likitolewa na Benki hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela alisema malengo ya semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wanahisa wao pamoja na Watanzania wengine ili kuwajengea uwajibikaji wa kifedha na kuongeza ushiriki katika fursa za uwekezaji hususan katika soko la hisa la Da es Salaam.
Aidha, Nsekela alimshukuru Rais Mwinyi kwa ushirikiano wa kimkakati na mazingira mazuri ya biashara ambayo ndio chachu ya utendaji mzuri wa benki hiyo. Kadhalika, alimhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa Benki ya CRDB itaendelea kuwezesha uchumi wa Zanzibar kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo hususan katika kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za Uchumi wa Buluu.
Katika semina hiyo, mada mbalimbali zilijadiliwa, ikiwa ni pamoja na Ujumuishi wa Kifedha, Uwekezaji katika Hisa, Hatifungani ya Kijani ya Benki ya CRDB, Wosia na Mirathi, pamoja na Kinga dhidi ya Majanga.
Sehemu ya Wanahisa wakiwa katika Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB ambayo imefanyika leo katika Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuelekea Mkutano Mkuu wa Benki
hiyo utakaofanyika hapo kesho.
wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuelekea Mkutano Mkuu wa Benki
hiyo utakaofanyika hapo kesho.Picha na Othman Michuzi.
wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuelekea Mkutano Mkuu wa Benki
hiyo utakaofanyika hapo kesho.