TANESCO MKOA WA DODOMA WAAHIDI WANANCHI WAKE UPATIKANAJI WA UMEME WA UHAKIKA

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Meneje wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania wa Mkoa Dodoma Mhandisi Donasiano J Shamba amesema kuwa seriakli ilitoa fedha takribani Bilioni 53 ili kuongeza uwezo wa na upanuzi wa kituo cha grid cha kupoza umeme kilichopo Zuzu kutoka Megawati 48 hadi Megawati 200 kwa kiweka transformation mbili zenye uwezo wa MW 100 kila moja.

Na pia kuongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2022 Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyenga fedha Shilingi Bilioni 3.4 kuongeza transifoma ya pili yenye uwezo wa Megawati 12 (MVA 15) Hii ni katika upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha mzakwe kinachohudumia visima vya maji kutoka megawati 8 hadi Megawati 20.

Mhandisi Donasiano ameeleza hayo Jijini Dodoma katika mkutano wake na Wanahabari uliofanyika mape.a leo hii May 17,2024 wakati akielezea Mafanikio ya Tanesco Mkoa wa Dodoma ndani ya miaka Mitatu tatu ya uongozi wa Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Upanuzi wa kituo cha gridi cha kupoza umeme cha Zuzu kutoka Megawati 48 hadi Megawati 200,mwaka 2020 kituo kilikuwa na uwezo wa MW 48 tu kikiwa na transfoma 2 zenye uwezo wa MW 24 kila moja sawa na megawati 48 na mahitaji ya juu ya umeme Megawati 32. Serikali ilitoa fedha Dola za kimarekani milino 23 sawa na bilioni 53 kuongeza uwezo wake kufikia MW 200 kwa kuweka transfoma mbili zenye uwezo wa mg 100 kila moja sawa na MW 200”.

“Mahitaji ya watumiaji wa umeme katika Mkoa kutika kituo hiki yameendelea kuongezeka kutoka MW 32 mwaka 2020 hadi MW 63 mwezi March 2023. Kituo hiki cha Zuzu kinahudumia Jiji la Dodoma, Wilaya ya Chamwino,Wilaya Kongwa,Wilaya ya Bahi,Wilaya ya Mpwapwa na Wilaya ya Gairo (Mkoa wa Morogoro)”.

“Upanuzi wa kituo kupoza umeme cha Mzakwe kinachohudumia visima vya maji kutoka Megawati 8 hadi Megawati 20, Kituo hiki kinapoza umeme kwaajili ya visima vya maji vya mzakwe na kutoa huduma kwa wananchi wa kata ya Mndemu Wilaya ya Bahi,Mwaka 2021 kituo cha mzakwe kilikuwa na transfoma moja yenye uwezo MW 8 tu hivyi endapo ikipata hitilafu yeyote ilisababisha ukosefu wa huduma ya umeme na kupelekea ukosefu mkubwa wa huduma ya maji katika Mkoa “.

“Katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitenga fedha Shilingi Bilioni 3.4 kuongeza transfoma ya pili yenye uwezo wa MW 12 (MVA 15). Mradi ukakamilika ndani ya mwaka mmoja mwishoni mwa mwaka 2022”.

Aidha Mhandisi Shamba amesema kuwa katika kuboresha upatikanaji wa umeme na kuchagiza uwekezaji Serikali ilitoa fedha ya dharula kiasi cha Shilingi Bilioni 2.6 kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme ya kutumia nguzo za zege yenye urefu wa Km 25.5 kutoka kituo cha kupoza umeme cha grid Zuzu kwenda Nala ili kuboresha upatikanaji wa umeme katika eneo hilo la viwanda.

“Eneo la Viwanda Nala halikuwa na umeme wa uhakika na hivyo wawekezaji wengi kutovutiwa kuwekeza katika eneo hilo, hivyo Serikali ilitoa fedha ya dharula kiasi cha Shilingi Bilioni 2.6 kwaajili ya ujenzi wa njia ya umeme ya kutumia nguzo za zege yenye urefu wa Km 25.5 kutoka kituo cha kupoza umeme cha grid Zuzu kwenda Nala ili kuboresha upatikanaji wa umeme katika eneo hilo la viwanda”.

“Uwezo wa njia hiyo iliyojengwa ni MW 40,hivyo viwanda vingi vinaweza kuanzishwa eneo hilo bila kuwa na tatizo la laini kuzidiwa . Mradi umekamilika kwa asilimia 100 na unafanya kazi toka Disemba 2022, Ujenzi wa njia hii umesababisha njia za umeme zinazoingia eneo hili la viwanda kuwa mbili ili kuwa na mbadala endapo kunatokea shida kwenye njia moja wapo”.

Pia amejivunia kwa mafanikio ya kupunguza mlundikano wa wateja walikuwa wakitaka huduma mbalimbali ikiwemo za uunganishiwaji wa umeme katika ofisi zao baada ya uanzishwaji wa teknolojia ya mfumo wa Nikonekt kufanya kazi.

“Tanesco Mkoa kwa kutumia mfumo wa nikonekt kuanzia Julai 2022 hadi 15.05.2024 uliweza kupokea maombi 109,930 ambapo katika hayo maombi ni 66.86% walitumia,94.6%walitumia mtandao kuomba huduma ya umeme wakati ni 5.4% tu ndio waliotembelea ofisi zetu kwaajili ya kupata huduma hiyo”.

Haya ni mafanikio ya utekelezaji wa Miradi na shughuli za Serikali katika Sekta ya umeme kipindi cha miaka mitatu ya Serikalini ya sita Mkoa wa Dodoma.

Related Posts