Mada kadhaa zimewasilishwa katika mdahalo wa siku mbili ulofanyika Zanzibar na kuhuduhuriwa na viongozi wa asasi za kiraia nchini, na wanasiasa kutoka vyama vikuu vya siasa, viongozi wa dini , wanaharakati, waandishi wa habari na wataalamu kutoka Afrika Kusini na Kenya pamoja na mabalozi kutoka nchi za nje.
Wajumbe walijadili mada kadhaa zinazoangazia muelekeo wa kupata katiba mpya ya Tanzania, uimara wa serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar na kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwakani 2025.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Benson Bagonza amesema historia ya nchi yetu ni kudai bila ya kumwaga damu.
Dkt Benson Bagonza ameongeza kuwa. “Tuliingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila ya kumwaga damu, tumeulinda muungano wetu bila ya kumwaga damu na sasa tunahitaji katiba mpya bila ya kumwaga damu.”
Wajumbe wengi wameonesha kuwa na shauku ya kutaka katiba mpya na kueleza kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Samia Suluhu Hassan ameonesha utayari, lakini baadhi ya wasaidizi wake ambao hawakutajwa wanakwamisha au kuchelewesha mabadiliko kadhaa ya kisiasa ikiwemo upatikanaji wa katika mpya.
Wanasheria wabobezi kutoka Afrika Kusini DK Albie Sachs aliyesaidia kuandikwa kwa katiba ya Afrika Kusini, na Mama Bi Jill Cotrell Ghai Kutoka Kenya walielezea uzoefu wao ambapo kila mmoja alisema udhati, umoja wa wanaharakati, na nia njema vinahitajika kufikia malengo, na kwamba pia harakati za katiba zinahitaji uvumilivu mkubwa.Mjadala kuhusu sheria ya uchaguzi Tanzania bado wafukuta
Mwanaharakati wa haki za binadamu, Dk Helen Kijo Bisimba anaelezea walichojifunza kutoka kwa wanaharakati wenzao wa Kenya na Afrika Kusini.
“Kwa mfano Kenya umeona walikuwa na tume ya serikali lakini kulikuwa na tume yao ya wananchi baadae ikiunganishwa ikawa moja na pia Afrika Kusini hivyo hivyo kutokana na historia yao lakini pia watu walihusika zaidi katika mambo ya upatanishi na nini na walihusika zaidi ya ikatokea lakini huku kwetu tumekuwa tunategemea sana watawala na mashirika ya kiraia tunaenda kidogo mara wanashirika wanasiasa kidogo tunaacha na hiyo ndio tofauti yetu na wanasiasa sisi na wao.”
Baadhi ya vijana waliohudhuria kongamano hilo walikuwa na haya ya kusema. Sabrina Soud kutoka Taasisi ya Thamini “Jamii nimejifunza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa vijana kutoka sekta tofauti kama ni wanafunzi au kutoka kwenye jamii kushiriki katika mikutano kama hii na kidemokrasia.”
Wisal Mohammed kutoka Taasisi ya ZAFAYCO, “katika mkutano huu nimegundua kuwa ipo haja kuwaleta pamoja viongozi wa kidini kisiasa na asasi za kiraia na kuwaweka pamoja aktika kupambania demokrasia na maendeleo ya kitaifa kwa ujumla.”Hisia za vyama vya siasa Tanzania kuhusu demokrasia ya nchi
Mabalozi Bw Michael Battle kutoka Marekani, Bi Metter Dissing Spandet Kutoka Denmark, Bw Didier Chassot Kutoka Switzerland, and Bw David Concar Kutoka Uingereza ambao walihudhuduria kongamano hilo, walisema Tanzania imekuwa ikipiga hatua nzuri katika kuimarika demokrasia na utalawa bora na kwamba nchi zao zitaendelea kuungamkono jithada hizo.