KATIBU Mkuu wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Kigoma, Aq Qassim Anasi amesema idadi ya watoto wanaojifunza mchezo huo imeongezeka.
Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka Kigoima, katibu huyo alisema mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa mara mbili kwa wiki, Jumamosi na Jumapili na wazazi wamekuwa wakiwaruhusu watoto kuja kushiriki katika Uwanja wa Lake side.
“Kwa kweli wazazi wa vijana hao wameonyesha nia ya kutaka vijana wao wajifunze mchezo huo,” alisema Anasi.
Wakati huo huo, alisema uongozi wa kikapu wa mkoa huo unatarajia kukutana kujadiliana kuhusu ushiriki wao katika mashindano ya CRDB Taifa Cup, baada ya kupokea barua ya ushiriki mwaka huu na moja ajenda watakayoijadili ni kutafuta fedha za maandalizi ya timu ya mkoa huo.
Mashindano hayo yamepangwa kuanza Juni 19-29, katika viwanja vya Chinangali mkoani Dodoma.