Wizara ya Mambo ya ndani yafanya kikao Maalumu na Viongozi wa Dini kujua namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu

Katika kukabiliana na matukio ya uhalifu yanayotokea katika jamii tunayoishi Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanya Kikao Maalumu na Viongozi wa Dini lengo ikiwa kuhusisha kundi hilo katika kudhibiti matukio ya mauaji,mmomonyoko wa maadili,matumizi ya dawa za kulevya na matukio yanayoweza kuvuruga amani ya nchi.

Akizungumza katika Kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya wizara Mtumba jijini Dodoma,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuisaidia serikali katika kudumisha amani na usalama huku akiwaomba kutochoka kutoa ushauri kwa serikali katika kudhibiti matukio hayo.

Wakizungumza wakati wa kikao hicho viongozi hao wa dini akiwemo Sheikh Abubakar Zubeir,Mufti Mkuu wa Tanzania, Askofu Mkuu Gervais Nyaisonga,Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu Alex Malasusa,Mkuu wa KKKT wamesisitiza uwepo wa amani ndio nguzo ya maendeleo na wakiishukuru wizara kuona ipo haja ya kuwahusisha katika kudhibiti masuala ya uhalifu nchini.

Related Posts