Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

 

WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea uwezo Jeshi la Uhifadhi nchini kwa njia mbalimbali ikiwepo ya utowaji wa mafunzo mengi na ya mara kwa mara kwa Makamishna, maafisa na askari wa Jeshi hiko. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uratibu wa Jeshi la Uhifadhi, ACC Fidelis Kapalata, alipokuwa akifunga mafunzo ya uchunguzi wa kifedha ili kudhibiti utakatishaji fedha haramu unaotokana na uhalifu dhidi ya wanyamapori na mazao ya misitu.

ACC. Kapalata ameongeza kuwa Jeshi la Uhifadhi linaumuhimu Mkubwa katika kuhakikisha utajiri wa Maliasili zilizopo nchini chini wa Wizara ya Maliasili na Utalii unalindwa, hivyo mkakati wa kuwajengea uwezo watendaji wa Jeshi hilo ni hatua muhimu ya kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa kwa maslai mapana ya watanzania na Taifa kwa ujumla.

Aidha ACC. Kapalata ametoa wito kwa Taasisi zote za Jeshi la Uhifadhi kuhakikisha wanachangamkia fursa hizo za mafunzo yatakayo tolewa mara kwa mara kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama nchini pamoja na wadau wa uhifadhi, ili kuimarisha uwezo wa watumishi wa taasisi hizo.

Pamoja na kuwapongeza washiriki wa mafunzo hayo, ACC. Kapalata amewasihi wakayaishi yote waliojifunza kwa siku nne kwani kwa kutofanya hivyo watakuwa hawajawatendea haki watoa mada, mwajiri na mfadhili wa mafunzo hayo, hivyo wanapaswa kuyafanyia kazi kama ilivyo kusudiwa.

“Nishukuru sana wawezeshaji wote kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) na Jeshi la Polisi. Niseme tu kwa dhati kabisa tunathamini sana sana juhudi za kila siku mnazofanya za kusaidia Jeshi la Uhifadhi kwenye maeneo na nyanja tofauti tofauti,” aliongeza ACC. Kapalata.

Washiriki wa Mafuzo hayo pamoja na mada zingine, wameimarishwa katika Utambuzi na ufuatiliaji wa mali (Asset identification and Tracing), Utumiaji wa taarifa za kiintelijensia katika kuchunguza makosa ya utakatishaji fedha, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizii (Use of financial intelligent Information related on Money Laundering,Terrorist Financing and proliferation Financing).

Related Posts