MAHAKAMA YA RUFAA YAFUTA HUKUMU YA MIKOPO CHECHEFU

 

Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Rufaa imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama kuu divisheni ya biashara katika moja ya kesi maarufu za mikopo chechefu baina ya kampuni ya State Oil dhidi ya Benki ya Equity kesi ambayo Mahakama Kuu hiyo chini ya Jaji Magoiga iliipa ushindi kampuni ya husika ambayo ilikopa dola milioni 18 (zaidi ya Shilingi Bilioni 45 za kitanzania) na kukataa kulipa kisha kukimbilia mahakamani
Ikiongozwa na majaji watatu Rehema Mkuye, Abraham Mwampashi na Zainab Muruke mahakama hiyo imeona kasoro kadhaa za kiuendeshaji wa kesi katika mahakama kuu divisheni ya biashara iliyofunguliwa na kampuni ya State Oil ikitaka mahakama itoe amri kwa kampuni hiyo kutokulipa kiasi cha shilingi bilioni 45 za kitanzania ilizokopa kwa kampuni ya Lamar ya Dubai na kudhaminiwa na benki ya Equty
Katika hukumu hiyo ambayo gazeti hili imepata nakala yake, majaji hao wanasema kuwa wametumia mamlaka waliyopewa kisheria ya kufuta hukumu na mwenendo mzima wa kesi hiyo na kuelekeza ianze kusikilizwa upya katika mahakama kuu divisheni ya biashara huku ikionyesha makosa kadhaa kubwa likiwa ni kutokushirikishwa kwa upande muhimu katika shauri hilo la Equity Benki ya Kenya
‘’Kiasi cha mkopo cha USD 18,640.000.00 kilitolewa na LAMAR kwa SOT(State Oil Tanzania) kupitia akaunti ya escrow iliyofunguliwa na EBK (Equity Bank Kenya) kwa jina lake. Baada ya hapo, EBK ililipa deni lote la SOT kwa EBT na benki zingine. EBK pia ilijilipa kamisheni ya USD 372,800.00 yenyewe, USD 750,000.00 kwa NISK kwa huduma za ushauri na udalali na USD 74,560.00 kwa serikali ya Kenya kama ushuru wa bidhaa na Salio lililosalia kwa SOT lilikuwa USD 736,899.74.’’ Inasomeka sehemu ya Hukumu hiyo.

Related Posts