TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, limechagiza vyema shamrashamra zinazoanza za Maadhimsho ya Siku ya Nyuki Duniani huku wanavyuo mbalimbali wa Jijini Dodoma wakifurahi, maonesho mbalimbali ya bidhaa zinazotokana na Nyuki pamoja na Maonyesho ya jukwaani kutoka kwa wasanii mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Akizungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo la aina yake, Kaimu Mkurugezi Msaidizi Uendelezaji Ufugaji Nyuki, Daniel Pancras, licha ya kuwapongeza wanavyuo na wanachi waliofika katika viwanja hivyo, ametoa wito kwa wananchi wote hususani wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo yatakayodumu kwa siku nne na kilele chake ni tarehe 20 Mei 2024 huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.