Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine Kasike leo Jumatatu amekutana na Mjumbe wa Kamisheni ya Siasa ya Chama cha FRELIMO, Alcinda António de Abreu na kukubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano kwa maslahi ya nchi zote mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kupitia mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi za Makao Makuu ya FRELIMO zilizopo jijini Maputo, Viongozi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Kwa upande mwingine, Balozi Kasike alikipongeza Chama cha FRELIMO kwa kumaliza mchakato wa kumpata Mgombea wake wa nafasi ya Urais kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 9 Oktoba 2024 ambapo Daniel Francisco Chapo aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho.