Billioni 38 kunufaisha wakulima nyanda za juu Kusini

Wafadhili kutoka Canada Wametoa bilioni 38 kwajili ya kusaidia shughuli za kilimo Nchini ili kuhumimili Athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Fedha hizo zimetolewa na Canada kupitia shirika la Care International Tanzania na mradi wake utakuwa wa miaka 6 katika wilaya za Iringa , Kilolo , Mufindi, Wangi’ombe pamoja na Mbarali .

Akizungumza baada ya kupokea ugeni wa wa Waziri qa Maendeleo ua Kimataifa wa Canada , Christina John ambaye pia ni meneja Mwandamizi wa Rasilimali na uhusiano wa Shirika la Care Tanzania amesema lengo ni kuongeza uzalishaji wa mkulima na kutunza mazingira.

Christina Amesema katika mradi huo wakulima wataunganishwa na Mamlaka ya Hali ya hewa TMA ili kufanya uamuzi wenye shauri kutoka kwao .

Naibu waziri wa Kilimo David Silinde ambaye alihudhuria uzinduzi wa mradi huo amesema serikali ya Tanzania imepokea msaada huo na unatarajiwa kuwanufaisha wakulima zaidi ya 175,282 huku ukiwanufaisha zaidi wanawake na Vijana.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada , Ahmed Hussein amesema Cananda ipo tiari kufadhili juhudi za utunzaji wa mazingira ili kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi .

Related Posts