MECHI ya Mei 20, itakayopigwa Uwanja wa Namungo, Morogoro, itakuwa ya kusaka nafasi kwa Namungo kupanda nafasi za juu kwa Mtibwa Sugar kuongeza pointi hata ikishinda itasalia nafasi ileile (mkiani).
Namungo imecheza mechi 27, imeshinda saba sare 10 na imefungwa 10, inamiliki mabao 22, imefungwa mabao 25 na imekusanya pointi 3, ipo nafasi ya nane, wakati Mtibwa ipo mkiani kwa pointi 20, katika mechi 27 iliyocheza imeshinda tano, sare tano, imefungwa 17, inamiliki mabao 27, imefungwa mabao 46.
Mzunguko wa kwanza mechi iliyopigwa Desemba 7, Uwanja Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi, Namung1-0 Mtibwa Sugar.
Timu hizo zina wachezaji wazoefu wanaoweza kumua mechi hiyo kwa upande wa Namungo FC baadhi ya ni Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Jacob Masawe na Pius Buswita.
Kwa Mtibwa, washambuliaji ni Charles Ilanfya, Rashid Juma, makipa Mohamed Mkaka na wa kigeni Justin Ndikumana, beki Oscar Masai, hivyo hautakuwa mchezo rahisi licha ya timu hiyo, kuburuzwa mkiani.
MISIMU MINNE NYUMA 2022/23
Namungo 2-2 Mtibwa Sugar (Agosti 15)
Mtibwa Sugar 1-1 Namungo FC (Desemba 16) 2021/22
Namungo 3-1 Mtibwa Sugar (Feb 6)
Mtibwa Sugar 2-4 Namungo (Juni 26) 2020/21
Mtibwa Sugar 1-0 Namungo FC (Oktoba 7)
Namungo 1-0 Mtibwa Sugar (Mei 12) 2019/20
Namungo 1-0 Mtibwa Sugar (Oktoba 23)
Mtibwa Sugar 1-1 Namungo (Mei 4).
Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema “Kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu, hakumanishi ndio mwisho wa kupambana kwetu, tunachotakiwa ni kushinda mechi zote, Namungo ina wachezaji wazoefu tutapambana nao.
Kwa upande wa kocha mkuu wa Namungo FC, Mwinyi Zahera amesema “Tunahitaji kupanda nafasi za juu, najua mchezo hautakuwa rahisi, ila wachezaji wangu wapo tayari kupambania pointi tatu, kutoka kwa Mtibwa.
Mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma ambaye aliwahi kuibuka mfungaji bora mara mbili (2003 na 2006), asema “Kiukweli Mtibwa ipo wakati mgumu, ingawa huo mchezo utakuwa mgumu, dakika 90 ndizo zitakazoamua.