Samatta abeba kombe Ugiriki – Mtanzania

Na Mwandishi Wetu

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta ametwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ugiriki akiwa na timu yake ya PAOK baada ya kuifunga Iris mabao 2-1 ugenini.

Ikiwa ni msimu wake wa kwanza na timu hiyo aliyojiunga nayo akitokea Fenabahce ya Uturuki, amehusika katika mabao sita, akifunga mawili na kutoa pasi nne.

Paok imemaliza kileleni na pointi 80 katika msimamo ya Ligi Kuu Ugiriki.

Related Posts

en English sw Swahili