Wananchi walalamika kuchapwa viboko na viongozi wa serikali

Wananchi wa kata ya Kidegembye halmashauri ya wilaya ya Njombe wamelalamikia kitendo cha baadhi ya viongozi wa Serikali ya kata hiyo kuwachapa viboko wanapo kosea jambo ambapo wameiomba Serikali pamoja na Chama kuchukua hatua dhidi ya jambo hilo.

Beatrice Msigwa na Luka Mangua ni miongoni mwa wakazi wa Kidegembye wameeleza hayo kwenye mkutano wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo wamesema baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwachapa viboko na kuwatoza faini kubwa kinyume na Sheria.

“Wananchi hatutendewi haki,utashangaa una tatizo lakini badala ya kufuatilia tatizo lake unaanza kupigwa viboko niombe mtusaidie yani mwananchi anapigwa anazimia hadi anaenda kulazwa”amesema Mangula

“Kuna siku vijana walisingiziwa wameiba Pikipiki na walipigwa mpaka mmoja akalazwa kituo cha afya na ile Pikipiki tuliambiwa ina thamani ya Milioni sita tukailipa”amesema Beatrice Msigwa

Baada ya kusikiliza kero za wananchi hao katibu wa Siasa na Uenezi wilaya ya Njombe Hitler Msolwa amewahakikishia wananchi hao hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidhi ya viongozi watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo kwa kuwa Chama kinafikisha malalamiko katika mamlaka husika.

Ayo TV inaendelea na jitihada za kumtafuta mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ili kupata ufafanuzi dhidi ya vitendo hivyo.

Related Posts