Ecobank Tanzania imezindua huduma ya utoaji wa Mikopo kwa watumishi wa umma ambayo inawalenga watumishi wote wa umma nchini ili kufikia malengo yao ambayo wamejiwakea na kuyakamilisha kwa uharaka na urahisi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Dr. Charles Asiedu amesema ni wakati sasa kwa benki hiyo kuwafikia watumishi wa Umma katika sekta mbalimbali nchini na kuwapatia huduma hii muhimu sana ya Mikopo ili kuinua vipato na maisha yao kwa ujumla.
“Si hivyo tu bali kwa watumishi wa umma ambao tayari wana mikopo kupitia taasisi zingine ya fedha, Ecobank itanunua mkopo yao na kuwapa nafasi ya kuongeza zaidi ili kuyafikia malengo yao.” Alisema Asiedu
Naye Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi, Bi. Ruth Mwaiselage amesema Ecobank Tanzania itatoa mikopo ya hadi millioni 125 kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za Serikali kwa riba ndogo kabisa ya asilimia kumina mbili (12% tu) ambapo mtumishi wa umma anaweza kukipa katika kipindi kisichozidi miaka saba. Mikopo hii itatolewa kwa haraka ndani ya masaa 24.
“Tunapenda kuwakaribisha watumishi wa umma kutoka taasisi mbalimbali waje Ecobank kujipatia huduma hii”. Alisema Bi. Ruth Mwaiselage
Amesema kuwa akaunti ya Watumishi wa Umma ni ya bure kabisa na haina makato ya mwezi. Mikopo hii ina Bima ya Maisha kumlinda mkopaji endapo kitatokea kifo, ulemavu wa kudumu au kupunguzwa kazi na namna ya kupata mkopo huu mtumishi wa umma anatakiwa kufungua akaunti ya Ecobank kupitia matawi yake yaliyopo Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Dr. Charles Asiedu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya utoaji wa Mikopo kwa watumishi wa Umma hapa nchini iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi, Ruth Mwaiselage akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyijipanga kuwahudumia watumishi wa Umma watakaohitaji mikopo ya Ecobank Tanzania wakati wa hafla iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo Kinondoni Jijini Dar es Salaam