MAKATIBU MAHSUSI WA OFISI YA RAIS -TAMISEMI WASHIRIKI MKUTANO 11 WA TAPSEA

OR – TAMISEMI, Mwanza

Makatibu Mahsusi wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI wameshiriki Mkutano wa 11 wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania(TAPSEA) unaofanyika Mkoani Mwanza.

Mkutano huo unawakutanisha Makatibu Mahsusi wa Tanzania Bara na Visiwani, Ofisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali lengo likiwa ni kukumbushana maadili ya kazi zao na kubadilishana uzoefu.

Akizungumza kwa niaba ya Makatibu Mahsusi Bi.Mwanakilima Nghomano amesema, mkutano huo utawasaidia kuwaongezea ujuzi na maarifa zaidi katika kutekeleza majukumu yao kutokana na mada watakazofundishwa.

“Sio tu kubadilisha uzoefu lakini pia tutafundishwa mada tofauti kutokana na majukumu yetu” amesema Mwanakilima

Aidha, mkutano huo unaofanyika mkoani Mwanza kuanzia tarehe 20 hadi 24 Mei, 2024 uliobebwa na kauli mbiu ya ” Mafanikio Huanza Uamuzi Bora wa Utendaji, Tutumie Muda Vizuri kwa Kufanya Kazi na Kuleta Tija”

Related Posts