Marekani yajitenga na safari ya anasa ya Rais Ruto

Nairobi. Serikali ya Marekani imefafanua kuwa haijaidhinisha malipo ya ndege binafsi ya Rais wa Kenya, William Ruto kwenda Marekani.

Rais Ruto ameanza ziara ya kiserikali ya siku nne nchini Marekani. Aliondoka nchini Kenya Jumapili, Mei 19, 2024.

Katika mujibu wa taarifa ya leo Jumanne, Mei 21, 2024, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi, Andrew Veveiros amesema: “Kwa kweli, Marekani haikulipia ndege ya Rais Ruto kwenda Marekani.”

Jibu hilo linafuatia habari ya kipekee iliyochapishwa na The Standard na KTN News leo, ikieleza ni kiasi kitakachowagharimu walipakodi kwa ziara ya Ruto Marekani.

Awali, gazeti la The Standard liliripoti kwamba walipa kodi watalipa gharama kubwa kwa safari ya Ruto. Ikulu imekodi ndege ya biashara ya Boeing 737-700 inayoendeshwa na kampuni ya Royal Jet ya Dubai.

Ndege hiyo ya kifahari yenye makao yake makuu Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, inahudumia soko la anasa kati ya UAE, Ulaya na Marekani. Gharama ya kukodi ndege hii ni kubwa takriban Dola za Marekani 18,000 (Sh46.7 milioni) kwa saa.

Safari ya ndege ya kwenda njia moja kutoka Nairobi hadi Atlanta, kama ilivyonukuliwa na Royal Jet, ni sawa na dola 748,600 (Sh1.94 bilioni) kwa safari ya saa 18. Ikizingatiwa safari ya Rais Ruto kwenda na kurudi Washington (safari ya karibu ya saa mbili), gharama ya jumla inaweza kuzidi Sh4 bilioni.

Saa moja ndani ya BBJ iliyoundwa na Edese Doret inaanzia dola 12,000 (Sh31.14 milioni), hadi kufikia dola 18,000 (takriban Sh46.7 milioni).

Kumsafirisha Rais na wasaidizi wake kutoka Nairobi hadi Atlanta, Marekani kunaweza kugharimu kati ya Sh572.28 milioni (makadirio ya chini) na Sh852.5 milioni (makadirio ya juu). Gharama zinazofanana zinatumika kwa safari ya kurudi.

Ingawa kuna machaguo mengine ya kibiashara, kama vile Shirika la Ndege la Kenya (KQ), uzoefu wa Ruto kwenye BBJ bado haulinganishwi.

Wakuu wa nchi za kigeni mara nyingi hukodisha ndege za mashirika ya nchi zao wakati wa ziara za serikali pale ndege zao za rais zinapokosa uwezo unaofaa. Katika kesi hii, safari ya Ruto ni mfano wa utajiri kwa gharama ya ajabu.

Kwa hiyo, wakati safari ya siku nne ya Rais Ruto nchini Marekani inapoendelea, mlipakodi atatakiwa kulipia safari ya rais ambayo inavunja kanuni za kibiashara, safari ambayo imejaa anasa na utata.

Ruto amesafiri  kwa mtindo unaoashiria ziara ya kwanza ya Rais wa Afrika nchini Marekani katika kipindi cha miaka 15.

Related Posts