Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza kuongeza muda wa siku tano, kwa vijana wenye sifa ya kuomba ajira kwenye jeshi hilo.
Katika tangazo lilitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania leo Mei 21,2024 limeeleza kuwa kutokana na changamoto ya mtandao iliyoendelea kujitokeza, hivyo kwa vijana wenye sifa na nia ya kujiunga na jeshi hilo zimeongezwa siku tano.
Mei 15, 2024 jeshi hilo lilitoa tangazo la kuongeza muda wa kuomba ajira na mwisho wa kutuma maombi hayo, ilikuwa ni leo Mei 21,2024.
“Kutokana na changamoto ya mtandao iliyoendelea kujitokeza mnatangaziwa kuwa vijana wenye sifa na nia ya kujiunga na Jeshi la Polisi zimeongezwa siku tano za kuendelea kutuma maombi,” imesema taarifa hiyo.
Kutokana na tangazo hilo hivyo tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya ajira ni Mei 26,2024 badala ya Mei 21,2024.
Ambapo kwa wanaotaka kufanya maombi wanatakiwa kutuma kupitia ajira.tpf.go.tz huku maelezo mengine yakiendelea kupatikana kwenye tangazo la awali la Mei 9,2024.