WATENDAJI WA SERIKALI TATUENI KERO ZA WANANCHI ACHENI KUJIHUSISHA NA SIASA- DC SAME


NA WILLIUM PAUL, SAME.

MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewaonya watendaji wa Serikali wajikite zaidi kwenye kutimiza wajibu wao kutatua kero za wananchi kikamilifu na kuwaacha wanasiasa wafanyekazi zao za siasa.

Kasilda amesema hayo wakati wa ziara yake kata Msindo kijiji cha Duma iliyolenga kusikiliza kero na kukagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho ambao umefikia hatua ya kunyanyua boma na mafundi wanaendelea na ujenzi.

Aidha amewasisitiza mafundi kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa kuhakikisha mradi unakuwa na matumizi endelevu kwa wananchi wa Kijiji cha Duma, lakini pia wajenge kwa kuzingatia taratibu zote zinazotakiwa kwenye utekelezaji wa mradi ya Serikali.

“Niwaombe wananchi wangu wa Duma lisimamieni jengo lenu hili ni mali yenu na kizazi chenu wasije watu hapa wakawatenganisha wakatengenenza propaganda itakayosababisha hii Zahanati isiwe na maslahi kwenu”..Alisema Kasilda.


Related Posts