YOUNG JONN AMVUTA KIZZ DANIEL NA SEAN PAUL KWENYE ALBUM YA “JIIGGY FOREVER”

MTAYARISHAJI wa muziki na msanii wa muziki kutoka lebo kubwa ya muziki nchini Nigeria, Chocolate City, Young Jonn anatarajiwa kuachia albamu yake ya kwanza, iitwayo ‘Jiggy Forever’

Jiggy Forever ni albamu itakayobeba ngoma zipatazo 16, ambapo ina ngoma kama ‘Hold On’ amefanya na rapa Sean Paul kutoka Visiwa vya Caribbean Jamaica, lakini pia amepita kwenye mitaa ya Lagos, Nigeria na ametoa shavu kwa mtu mzima Kizz Daniel na Seyi Vibes kwenye wimbo wa “Big Big Things” .

Mbali na hivyo pia albamu ya Young Jonn ‘Jiggy Forever’ inatajwa kuwa ni albamu bora ambayo italeta mapinduzi makubwa ya kiburudani kwani inatajwa kusheheni mastaa wakubwa wa muziki duniani kama vile Zlatan, Don Jazzy bila kumsahanuYa Levis.

Vile vile Young John amatarajia kufanya ziara yake ya kikazi katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki, kuanzia nusu ya pili ya mwaka 2024 kwa lengo la kuhimiza ushirikiano katika soko la muziki wa aina ya Afrobeats.

Mwaka 2021 Young Jonn aliingia rasmi kwenye tasania ya muziki (Uimbaji) kutoka kuwa mtayarishaji wa muziki, hii ni baada ya kusaini Mkataba wa Kurekodi, lebo Chocolate City Music.

Na baada ya hapo akatoa kazi yake ya kwanza iitwayo ‘Love Is Not Enough Vol. 1’ ambayo ilipata umaarufu mkubwa, na ikafanyiwa remix ya wimbo wake wa kwanza uitwao “Dada”, remix hii alifanya na mtu mzima Davido, ambapo ikapelekea kutoka kwa kazi nyingine ya Love Is Not Enough Vol. 2.

Related Posts