Ayatollah Khamenei aongoza wairan kumuaga Raisi

Kiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza mjini Tehran, ibada ya kumswalia na kutoa heshima za mwisho kwa rais Ebrahim Raisi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).

Ibada hiyo pia imewahusisha waziri wake wa mambo ya nje Hossein Amir-Abdollahian na maafisa wengine wa serikali waliofariki dunia kufuatia ajali ya helikopta Magharibi mwa Iran.

Ibada hiyo imefanyika katika chuo kikuu cha Tehran ambako majeneza ya viongozi hao yalifunikwa kwa bendera ya Taifa na picha zao kuwekwa juu yake.

Kaimu rais wa Iran, Mohammad Mokhber aliyesimama muda wote kando na Khamenei alibubujikwa machozi wakati ibada hiyo ikiendelea.

Kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh alishiriki kwenye ibada hiyo. Haniyeh amesema amefika katika ibada hiyo kutoa risala zake za rambirambi pamoja na watu Palestina kwa Iran kwa kuwapoteza viongozi wao muhimu.

Iran imekuwa ikiiunga mkono Hamas katika vita vyake na Israel katika Ukanda wa Gaza.

Related Posts