‘Ayra Starr ni mwanamuziki nyota anayechipukia lakini anag’ara kimataifa’Tiwa Savage

Mwimbaji wa Nigeria, Tiwa Savage afichua kwamba anavutiwa na Ayra Starr kwa sababu ya uzoefu wake kwenye kazi kuwa muimbaji anaemkubali.

Alibainisha kuwa Starr ameendelea kung’ara kwenye anga ya muziki duniani licha ya ukosoaji unaoletwa kwake na Wanigeria kuhusu uvaaji wake.

alisema, “Nampenda Ayra [Starr]. Ninavutiwa naye. Yeye ni wa kushangaza na mtu anayeishi maisha ya kweli, pia. Inanitia moyo kwa sababu nilipoanza, nilikosolewa sana kwa kuvaa nguo zenye kuvutia zikiitwa za uchi sana na maneno yangu kuwa hatari sana.

“Kwa hivyo, nikiona mtu, kamaAyra sasa … Nikimwona amevaa sketi fupi kama wanavyosema [wakosoaji], ni kama nasema, ‘Ifanye iwe fupi.’

“Na anaonekana kushangaza, ana talanta sana. Ndio, yeye ni nyota.”

Related Posts