John Mongela akiongea na watumishi wa CCM na Jumuiya zake mkoa wa Tanga

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu John V.K Mongella amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tanga na kuzungumza na Watumishi wa CCM na Jumuiya zake, katika kikao hicho amewaeleza Watumishi juu ya suala la Uwajibikaji ni jambo kila mmoja, kila Mtumishi ahakikishe anasimama na Katiba, Miongozo na taratibu zilizowekwa.

Amewakumbusha kuandaa mpango kazi wa majukumu yao ya kila siku, Watumishi wakumbuke mwaka 2024 ni mwaka wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni vema wakajipanga na kushirikiana ili CCM iweze kushinda kwa kishindo.

Aidha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga kinatoa shukrani kwa Mweyekiti wa CCM na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea Fedha nyingi za miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya 9 za Mkoa wa Tanga.

Related Posts