KAMPUNI YA HEINEKEN YAUNGANA NA KAMPUNI YA DISTELL, KUSHEHEREKEA MEI 25, 2024 JIJINI DAR

Meneja Mkazi hapa nchini wa kampuni ya HEINEKEN, Obabiyi Fagade, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saam leo Mei 22, 2024.

akizungumzia kampuni hiyo kuwa imeshakamilisha Manunuzi ya Kampuni ya Distell Group Holdings Limited (‘ Distell’) na Namibia Breweries Limited (‘NBL’). Kulia ni Meneja Masoko wa Heineken nchini, Lilian Pascal na kushoto ni 

Meneja Masoko wa Heineken nchini, Lilian Pascal akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 22, 2024. Na kushoto ni Meneja Mkazi hapa nchini wa kampuni ya HEINEKEN, Obabiyi Fagade.

* Profesa Kitila Mkumbo Mgeni rasmi

KATIKA Kusheherekea hatua mhimu ya Kampuni ya Heineken kukunua Kampuni ya Distell Group Holding Limited (Distell) na Namibia Breweries Limited inatarajia kuzindua Jalada lake jipya la bidhaa  jumamosi ya Mei 25, 2024 jijini Dar es Salaam.

Meneja Mkazi hapa nchini wa kampuni ya HEINEKEN, Obabiyi Fagade, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saam leo Mei 22, 2024, amesema kuwa kampuni hiyo imeshakamilisha Manunuzi ya Kampuni ya Distell Group Holdings Limited (‘ Distell’) na Namibia Breweries Limited (‘NBL’).

Katika Sherehe hiyo itakyofanyika Mei 25, 2024 Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ambapo atajumuika na wadau wengine mashuhuri na viongozi wa tasnia mbalimbali.

Licha ya tangaza Jarida Kununua Kampuni ya Distell na Namibia Breweries amesema kuwa Jalada jipya lina aina nyingi za bidhaa zinazotumia jina la ‘HEINEKEN Beverages, na linaonesha ubora wa hali ya juu kwa watumiaji mbalimbali.

Akizungumzia kuhusiana na dhamira ya kampuni hiyo , Fagade amesema kuwa Vinywaji vya kampuni hiyo vina ya ubora aina yake kwa watumiaji.

“Ununuzi wa hivi majuzi ambao unaongeza zaidi ya Euro bilioni 1 katika mapato halisi na Euro milioni 150 kama faida ya uendeshaji ambapo umeonesha

ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Tumepewa nafasi ya kipekee sio tu kufikia watu wengi zaidi kutokana na upanuzi wa kampuni yetu lakini pia kutengeneza nafasi nyingi za kazi na kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na ajira.” Amesema Fagade

Kwa Upande wa Meneja Masoko wa Heineken nchini, Lilian Pascal amesema kuwa Heineken kwa sasa inapatikana katika masoko 114, na kuuzwa katika nchi zaidi ya 180 ikiongoza katika tasnia ya Vinywaji nchini Tanzania.

Amesema kutokana na uwepo wa masoko mengi zaidi lakini wataendelea kuvumbua na kupanua wigo wa jalada lake ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja wake.

Related Posts