Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu amemtaka mkandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya wizara hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba kuwasilisha mpango kazi wa mradi huo baada ya kuwepo kwa ucheleweshaji wa umalizaji wa mradi huo ambapo hapo awali ulipaswa kumalizika oktoba mwaka jana na kuongezewa muda wa makabidhiano kuwa mwezi huu mwishoni lakini hadi sasa hakuna dalili za kukabidhiwa mradi huo kwa muda ambao mkandarasi aliomba kuongezewa.
Akizungumza baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi huo,Katibu Mkuu Ally Senga Gugu amesema mapokeo ya fedha za mradi kutoka Wizara ya Fedha yamekua mazuri lakini kwanini kumekuwepo kusuasua kwa mradi huo huku akimtaka Meneja Mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) kuwasiliana na kumsimamia mkandarasi ambae ni Shirika la Nyumba la Taifa ili aweze kumaliza mradi huo ili wizara waweze kukabidhiwa jengo likiwa limekamilika.
‘Hii ni taswira labda anaetenda kazi na anaesimamia kazi mawasiliano hayapo vizuri,aidha hamsikilizi au aambiwi kwasababu msimamizi anasema anatoa maelezo kwa kila namna lakini mtendaji anaongea lugha tofauti,inakuaje kifaa kikubwa kama lifti kinakuja kinafungwa bila kuwepo usimamizi wowote na hakuna zuio lolote,leo tunatakiwa tupandishwe lifti hii ni kama kitu kilifungwa usiku alafu asubuhi mkashtukia kimefungwa,kwahiyo bado aitupi taswira nzuri ya eneo lenu la kazi jinsi mnavyosimamiana kazi sasa tutoe maelekezo hilo lifanyiwe kazi ipasavyo,na kuna mambo yapo kwenye ngazi ya wizara tutaongea na sekta nyingine ili kuhakikisha mradi wetu unatimia nachowaomba wasilisheni mpango kazi ili tuone mtamalizaje ndani ya wakati uliobakia ambao ni muda mfupi sana bado siku kumi tu’ alisema Katibu Mkuu Ally Senga Gugu
Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wakati wa ziara hiyo,Mhandisi wa Mradi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa(NHC),Peter Mwaisabula amesema ni kweli awakamilisha asilimia mia ya kazi za nje kama sasa hivi kazi ya ujenzi wa uzio bado imesimama kwa sababu chuma zilichelewa kufika na kuhusu kuweka vitofali tumebakiza sehemu ndogo na tuna hakika kufikia mwisho wa mwezi zile kazi za msingi tutakua tumezimaliza na tumechukua maelekezo yako kiongozi na tutayafanyia kazi.
Naye Msimamizi wa Mradi anaetokea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Iddy Msangi alisema maelekezo ya serikali kutoka ofisi ya Waziri Mkuu na kutotoa kipaumbele cha kuongezewa muda kwa mkandarasi anaeshindwa kumaliza kazi zake kwa wakati huku akielezea mud awa kuisha mradi na jinsi mkandarasi anavyosuasua kumaliza mradi kwa wakati.
Mradi huo wa Ujenzi wa Ghorofa Tano ni moja ya miradi ya Maofisi ya Wizara yanayojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba,jijini Dodoma na Katibu Mkuu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani amekua akiipatia wizara hela ya kugharamia mradi huo kila wizara inapoomba fungu hilo.
Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa(NHC),Peter Mwaisabula akitoa maelezo ya lifti kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Ally Senga Gugu(wanne kushoto) wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya wizara hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba,wengine ni wahandisi wa mradi na viongozi wa idara na vitengo walioongozana na Katibu Mkuu wakati wa ukaguzi uliofanyika jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu(katikati) akitoka kukagua utengenezaji wa milango inayowekwa kwenye jengo la Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya wizara hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba,wengine ni wahandisi wa mradi na viongozi wa idara na vitengo alioongozana wakati wa ukaguzi uliofanyika jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi