Mwanamume wa Uingereza aliyetuhumiwa kuipeleleza China akutwa amefariki katika bustani

Mwanamume anayeshutumiwa kusaidia mamlaka ya Hong Kong kukusanya taarifa za kijasusi nchini Uingereza amefariki katika hali isiyoeleweka, polisi wa Uingereza waliripoti Jumanne (Mei 21.)

Matthew Trickett mwenye umri wa miaka 37 alikuwa miongoni mwa wanaume watatu walioshtakiwa mapema mwezi huu kwa kukubali kushiriki katika kukusanya taarifa, ufuatiliaji na vitendo vya udanganyifu ambavyo vina uwezekano wa kusaidia idara ya kijasusi ya Hong Kong kuanzia mwishoni mwa 2023 hadi Mei 2 mwaka huu.

Waendesha mashtaka waliendelea kudai kwamba mshtakiwa alilazimisha kuingia katika anwani ya makazi ya Uingereza mnamo Mei 1.


Serikali ya Hong Kong iliitaka Uingereza kutoa maelezo kamili ya madai hayo na kulinda haki za Yuen, ambaye ni meneja wa ofisi ya Ofisi ya Uchumi na Biashara ya Hong Kong mjini London.

Ubalozi wa China huko London na serikali ya Hong Kong hawakujibu mara moja maombi yaliyotumwa kwa barua pepe Jumatano ya kutoa maoni juu ya kifo cha Trickett.

Trickett, ambaye alitoka eneo la Maidenhead, alikuwa mwanamaji wa zamani wa Kifalme na alikuwa amefanya kazi kama afisa wa kutekeleza uhamiaji wa Uingereza. Pia aliripotiwa kuwa mkurugenzi wa shirika la usalama.

 

Related Posts