Tanzania yafungua milango ya ushirikiano na Indonesia katika Sekta ya Maji

Waziri wa Maji Tanzania, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ambaye yuko nchini Indonesia kumwakilisha Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kongamano la 10 la Maji Duniani, amefungua
milango ya ushirikiano kati ya Sekta ya Maji Tanzania na Sekta ya Maji Indonesia.

Wakizungumza katika mkutano wa upili, Waziri Aweso na Mhe. Hadimuljono, Waziri wa masuala ya maji Indonesia wamekubalina kushirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na teknolojia za mita za malipo ya kabla, uendelezaji wa maji chini ya ardhi, uimarishaji wa Taasisi na huduma za maji, pamoja na kubadilishana uzoefu kupitia Chuo cha Maji na Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 22 Mei Bali nchuni Indonesia abampo rasmi Mheshimiwa Aweso amehitimisha ziara yake.

Mhe. Aweso amemkaribisha Mhe. Hadimuljono, nchini Tanzania.

Related Posts