Timu za Tanzania za wanawake na wanaume (U15) zinazoshiri michuano ya African Schools Football Championship 2024 inayoendelea Zanzibar, zimefuzu nusu fainali ya mashindano hayo.
Timu ya wanawake imefuzu baada ya kushinda mechi zote mbili kwenye kundi A, lenye timu tatu na mchezo wa kwanza jana, iliifunga Morocco bao 1-0, mapema leo imeshinda dhidi ya Congo kwa bao 1-0 na hivyo kuvuna pointi sita.
Timu ya wanaume pia imefuzu baada ya kuvuna alama nne katika mechi mbili na ilityoka suluhu dhidi ya Senegal jana na mapema leo imeifunga Uganda bao 1-0.
Timu zote zitasubiri timu zitakazoongoza kundi B lenye timu za Afrika Kusini, Benin, Guinea na Libya kwa wanaume na kwa wanawake kundi B lina Afrika Kusini, Togo, Gambia na Uganda.