11 wafariki dunia baada ya mtambo wa Kiwanda cha Mtibwa Sugar kupasuka

WATU 11 wamefariki dunia huku watatu wakijeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 23 Mei 2024, kwenye kiwanda cha uzalishaji sukari cha Mtibwa (Mtibwa Sugar), kilichopo mkoani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, Alex Mkama, amesema watu watatu kati ya 11 waliofariki ni raia wa kigeni.

Amesema ajali hiyo imesababishwa na hitilafu ya umeme iliyotokea majira ya saa 7.30 usiku wakati wakiendelea na majukumu yao.

Naye Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Morogoro, Shaban Marugujo, amesema hitilafu hiyo ya umeme ilisababisha bomba la kusafirisha mvuke kupasuka na kusabisha vifo vya watu hao.

“Waliofariki wote ni wanaume, ajali ilitokea usiku wa kuamkia leo wakati wapo kiwandani wanatekeleza majukumu yao,” amesema Marugujo. Tanzania kufungua vituo 100 vya Kiswahili kimataifa.

Related Posts