ADHMA YA SERIKALI AWAMU YA SITA YA SAMIA NI KUJENGA UCHUMI IMARA- MAJALIWA.

 

” Ni adhma ya serikali ya awamu ya sita ya hapa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga uchumi imara kupitia biashara na uwekezaji, lakini vilevile serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaamini kuwa taasisi zote za serikali zinazowezesha biashara na uwekezaji hapa nchini pamoja na sekta binafsi zitakuwa na mchango mkubwa katika kutimiza adhma hii, na kwa kuwa taasisi zote binafsi zipo hapa, taasisi za serikali zipo hapa chini ya TIC zitapata nafasi ya kueleza mkakati uliopo ndani ya nchi, fursa tulizonazo ndani ya nchi na namna ambavyo tunawakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uganda” .

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye ni mgeni rasmi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji Kati ya Uganda na Tanzania akizungumza katika kongamano hilo linalofanyika jijini Dar es Salaam.

Related Posts