Hospitali ya CCBRT yaungana na wanawake kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ya uzazi

Kila mwaka ifikapo tarehe 23 Mei, dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ya uzazi, ambapo kwa mwaka huu wa 2024, siku hiyo kitaifa inaadhimishwa mkoani Arusha.

Wanawake wanaoendelea a matibabu ya fistula hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na watoa huduma wao nao pia  wameadhimisha siku hii ya kimataifa ya kutokomeza fistula.

Lengo la maadhimisho haya ni kuhamasisha jamii, kupanua wigo wa kuhudumia wagonjwa wa fistula, kuimarisha ubia, na kuweka pamoja raslimali za kukabiliana na tatizo la fistula kama sehemu ya mpango mpana wa kuboresha huduma za afya ya uzazi.

Hospitali ya CCBRT ni mdau mkubwa katika mapambano dhidi ya fistula hapa nchini, hivyo wameungana na wadau wenzao huko na Arusha lakini pia wanawake wenye ugonjwa huo wanaondelea na matibabu hospitalini hapo pamoja na watoa huduma wao wameadhimisha siku hiyo kwa kujumuika pamoja na kupeana tarifa mbalimbali juu ya changamoto za ugonjwa huo.

Daktari kutoka kitengo cha afya ya uzazi mama na moto katika hospitali ya Deüel Michael CCBRT Justin Nkato, ameeleza kuwa Fistula ni tundu lisilio la kawaida kati ya njia ya uzazi na kibofu cha mkojo au njia ya haja kubwa na tundu hili husababishwa nauchungu wa muda mrefu na uzazi pingamizi wakati wa kujifungua bila msaada.

    “Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 hospitali ya CCBRT imefanya upasuaji wa akina mama wenye shida ya fistula wapato 1,350 a kwa kipindi cha mwezi wa kwanza had wa nne mwaka huu wagonjwa wa fistula wapato 126 wamefanyiwa upasuaji kwenye hospitali ya CCBRT pekee.”

Kwa upande wake mmoja wa wanawake weye fistula walioko hospitalini hapo Eva Ndala Miaka 33 ameishukuru hopsitali ya CCBRT kwa msaada wao huo na kusema; “nilipopata ugonjwa huu ambao nimekaa nao kwa muda wa miaka mwili nilinyanyapaliwa sana na jamii inayozunguka ikiwemo kutelekezwa na mume wangu.

Ilifika wakati sikuweza hata kutoka ndani, siku moja nikiwa pale nyumbani alikuja baba mmoja aliyejitambulisha kwangu kuwa yeye ni balozi wa fistula katika eneo letu na hivyo, alinielezea juu ya uwepo wa matibabu ya bure ya ugonjwa wa fistula na ndipo anisafirisha hadi hapa, nashukuru sana kwa kweli maana baada ya kufika CCBRT niliwakuta wanawake wengi wenye tatizo kama la kwangu na hivi sasa mimi nimeshatibiwa ni mima wa afya na subiri kuruhusiwa kurejea nyumabni asanteni sana”

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni vunja Mnyororo: Zuia Fistula Tanzania, kauli mbiu hii inaweka msisitizo mkubwa wa kuzuia fistula kwa kukabiliana na mapungufu kwenye mifumo yetu ya afya na kwenye jamii ambayo hupelekea uzazi pingamizi ambacho ni chanzo kikuu cha fistula.

 

Related Posts