KAMA ilivyozoeleka kwa wachezaji wengi kuongelea historia zao na kusema walikuwa na vipaji tangu utotoni,wengine wakienda mbali zaidi na kusema wapo watu waliowaridhi katika familia zao ambao wanacheza au walicheza soka huko nyuma.
Lakini hii ya aliyekuwa Mwanafunzi wa ‘ New Era’ iliyoko Tabora Mjini ambako alikwenda kwaajili ya kupata Elimu ya Kidato cha Tano,akiwa anakiwasha sana Shule na kujizoelea umaarufu mkubwa akiwa na miaka 17 wakati huo.
Mwisho anapata bahati ya kwenda kufanya majaribio akiwa Shuleni,hapo nndipo historia yake ya maisha ilipoishia na kuamua kutazama upande wa pili wa shilingi wa maisha,jambo ambalo hajawahi kulijutia mpaka leo hii
Anaitwa Salum Kimenya Beki wa Tanzania Prison,analiambia Gazeti hili historia yake ya Soka ilivyoanza mpaka kufikia alipo akiweka rekodi ya kuitumikia Tanzania Prison kwa miaka 11 bila kuchezea timu nyingine.
Anasimulia jinsi alivyoanza safari ya soka mpaka kufikia hatua ya kuacha Shule na kuchagua mpira.Salum anaeleza na kusema,Kitu kilinivutia sana ni kipaji cha mpira kilinifanya nijaribu kuonesha nilichonacho kutokea kijijini.
“Mimi niligundua kipaji nikiwa na soma shule ya msingi katika Wilaya Urambo shule ya Msingi Ukombozi,badae nilifanikiwa kujiunga na sekondari katika shule ya Urambo sekondari iliyopo Urambo. Baadae Kipaji changu kiliendelea nilipojiunga shule ya New Era katika kidato cha tano iliyopo Tabora mjini. Hapa ndio kipaji changu kilizidi kuonekana nilipoanza kucheza katika timu za mitaani kama Chipukizi Umoja wa Wanafunzi Vijana wa Urambo.
Pia timu nyingi za mitaani Kama Walumba na Twiga zote za Urambo katika ligi za Wilaya na Mkoa nilikuwa mdogo kama kijana wa miaka 17,ndio nilielekea Mbeya kufaya ‘interview’ Tanzania Prisons badaye nilichagulia na kubaki hapa mpaka leo watu wamenifahamu Nchi nzima.”
Anasema “Kiukweli niliishia kidato cha tano Form Six sikumaliza maana ndio nilienda Mbeya kufanya majaribio nikitegemea ningeshindwa ningerudi shule, lakini nilichagulia nikaona nibaki niendelee na maisha ya mpira kwani hicho ndicho nilichokipenda zaidi.
Sijawahi kujutia maana niliowaacha shule sio wote wamefanikiwa naweza sema Mungu alipanga nipite njia hii kwani ilikuwa ndoto yangu kucheza Ligi kuu na Timu ya Taifa,”
Salum anaeitumikia kikosi cha Tanzania Prison tokea alipoanza safari yake ya soka anatoa siri ya kilichomfanya kukataa ofa nyingi zilizowahi kuja mezani ikiwemo ya Simba,Azam na anaeleza sababu ya yeye kuzipundua dili hizo.
“Simba na Azam kipindi hicho ziliwahi kunihitaji kweli lakini sikuridhika na ofa zao kipindi kile hazikunifurahisha maana nilikuwa mdogo na huku ndio nimepata kazi nikaona ofa ndogo nikaogopa kuharibu kazi yangu ya muda mrefu kwaajili ya dili ambalo linamwisho mfupi,kama inavyojulikana timu zenye ushindani mkubwa ubora ukipungua tu na kibarua chako kimefika mwisho.”
Anasema kwake hajutii kuchagua kuchezea soka kwani amepata faida kubwa zaidi ya hapo awali ambapo kama asingeuchagua basi asingekuwa alipo sasa.
“Mpira umenilipa kiukweli tofauti na mwanzo nilivyokua kwani nimeweza kufanya maendeleo makubwa na wakati huu nafanya kazi,nacheza mpira,na lima mashamba na kufanya biashara vyote hivi vikitokana na miguu yangu ya soka na kichwa kilichoamua kuchagua njia hii bila kujua kama ningetokea hapa.
Nilitaka kuwa Mwanasheria hivyo sidhani kama ningefanikiwa kwa ukubwa huu kwani ningechukua muda mrefu kusomea na sijui kama kazi ningeipata kwa urahisi mkubwa na kufanya yote niliyoyafanya sasa sisemi hivi kuwakatisha tamaa walioko huko ila naunzungumzia moyo wangu na bahati yangu kwa ujumla,”anasema Kimenya.
NILIWAHI KUTAMANI KUACHA SOKA
Anasema kuna kocha aliwahi kufundisha Prison wakati huo kwa sasa hawezi kumtaja jina na alimkatisha tamaa na kumfanya atake kuachana kabisa na mpira,anasimulia na kusema;
“Mchezaji sio vipindi vyote anakuwa sawa kiakili na kiuwezo kwahiyo nilikuwa kenye hali ambayo sio nzuri kiuwezo,basi kocha aliitumia hiyo kunikandamiza zaidi kwani hakuwahi kunipenda naweza kusema jambo ambalo linatokeahata kwenye maisha ya kawaida kuna mtu mwingine anaweza asikukubali bila kumuonyesha ubaya wowote.
Anasema jambo la furaha zaidi kwenye safari yake ya soka ni mafanikio aliyoypata, msimu aliofanya vizuri zaidi;”Msimu wangu mzuri zaidi katika soka ni ule wa nilifaya vizuri kuliko yote ni 2017/2018 nilikuwa na assisti nyingi sana na magoli 7 ya Ligi Kuu kama beki nilifanya vizuri.
Kutokana na nafasi ninayoichezea ni ngumu kufunga muda wote kama ilivyokuwa kwa washambuliaji ambao kwao kazi yao ni kufunga mabao na kiwako cha magoli nilichokuwa nacho msimu huo kwao ni kidogo,” anasema Kimenya.
KAZI YABADILI NDOTO ZA NJE
Kama ilivyo kwa wachezaji wengi kuwa na mipango ya kwenda kuchezea soka la kulipwa nje ya Tazania,kwake ni tofauti sana kwani analiambia gazeti hili kuwa hana huo mpango kabisa kwa sasa.
“Ndoto zangu kiukweli kwa sasa ni kupambana na soka la Bongo kwani tayri umri wangu wa kuwaza hivyo haupo tena na kilichobaki ni kujipambania na kazi na vile nilivyovianzisha nje na sio wa kwenda tena huko nasubiri kustafu serikalini basi Miaka 33 sina pakwenda nafikiria kurudi shule kujiongezea ujuzi kufika mbali katika kazi.”
Beki huyo anakiri kuwa kwa sasa Prisons haifanyi vizuri sana ijapo ipo nafasi ya tano katika msimamo wa ligi huku ikiwa imecheza mechi 21 na jumla ya alama 28 ikifunga,ikifungwa na kutoka sare mechi saba kwa ujumla.
“Hapana aise, kwani prisons hii tuliyopo tuliwahi shika nafasi ya nne mara mbili, ukiacha kucheza ‘playoff’ mara moja tu mwaka juzi hapo ndio kweli haikufanya vizuri na leo tunazungumza ipo nafasi ya tano.
Mimi ninachokiona iko sawa tu sema ligi imekua ngumu kwa sasa,kila timu ina uwekezaji mkubwa na hawa wadhamini wanaodhamini wanajitahidi kufanya ligi kuwa bora na jambo pekee ni kwamba wachezaji wenye ubora mkubwa wameongezeka kwa wingi na wote wanaofanya vizuri nawakubali.,” anamaliza Salum.