Mamia waandamana kwenye ofisi ya Netanyahu kushinikiza kuachiliwa kwa mateka

Waisraeli walikusanyika karibu na ofisi ya Netanyahu, kutafuta mpango wa kuachiliwa ndugu na jamaa waliotekwa nyara.

Mamia ya Waisraeli wameandamana mbele ya ofisi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu wakati wa mkutano wa baraza la vita wakitaka mateka wa Gaza waachiliwe huru.

Maandamano pia yalizuka katika miji kadhaa ya Israel baada ya video kuchapishwa ikiwaonyesha wapiganaji wa Hamas wakiwakamata wanajeshi wa kike wa Israel katika kambi ya kijeshi katika makazi ya Nahal Oz karibu na uzio wa Gaza Oktoba 7 mwaka jana.

Hamas ilisema katika taarifa yake kwamba “kipande cha video kinachosambazwa katika vyombo vya habari vya Israel ni sehemu iliyodanganywa na kuhaririwa, na ukweli wa maudhui yake hauwezi kuthibitishwa.”

Related Posts