RC Makonda atatua tatizo la umeme zahanati ya Leremeta -Longido

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ametembelea na kukagua utoaji huduma katika zahanati ya kijiji cha Leremeta ambapo amehoji kuhusu umeme unaopatikana katika zahanati ili kujua unawezesha mitambo yote kufanya kazi ipasavyo.

Katika majibu yake, uongozi wa zahanati hiyo umesema kuwa umeme hauridhishi kwakuwa ni single phase na moto unaopatikana ni mdogo hali inayopelekea hata kipimo kidogo cha damu kutoweza kufanya kazi.

Naye, Meneja TANESCO Longido Mhandisi. Lazaro Lenoi, mara baada ya kuulizwa na RC Makonda kuhusu uwepo wa umeme mdogo katika zahanati hiyo, amesema waliunganisha umeme wa single phase kwakuwa ndivyo mahitaji yao walivyoomba kutoka uongozi wa zahanati hiyo.

Kutokana na maji hayo, RC Makonda alimuhoji tena Mhandisi. Lazoro kuwa kwanini baada ya kupata malalamiko kwanini asingefika katika zahanati hiyo kushughulikia, jambo ambalo Meneja TANESCO amesema hajapokea malalamiko wala changamoto yoyote tangu walipounganisha umeme huo.

RC Makonda aliongeza swali kwa Meneja TANESCO na kumuuliza kwanini hakutumia utaalamu wake kutoa ushauri kwa uongozi wa zahanati hiyo ili kuwavutia umeme wa three phase, jambo ambalo amesema alishamueleza Mwenyekiti wa serikali ya kijiji ilipo zahanati hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji Mhe. Supuk Melita, mara baada ya kuulizwa na RC Makonda kuhusu ushauri huo, amekiri kuwa walipokea ushauri huo.

Mara baada ya kusikiliza pande zote mbili, RC Makonda ameamua kutoa kiasi cha fedha zaidi ya Tsh 100,000/= kuunganishwa kwa three phase katika zahanati hiyo ndani ya siku tatu.

Related Posts