Serikali yaanika mikakati maandalizi AFCON 2027

Serikali imesema inaendelea kufanya mazungumzo na wadau pamoja na wamiliki wa hoteli kubwa kwa ajili ya kuboresha hoteli hizo ili ziweze kukidhi viwango na hatimaye kuhudumia ugeni wa Fainali za Mpira wa Miguu Barani Afrika (AFCON 2027). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika mashindano hayo, Tanzania ni mwenyeji kwa kushirikiana na Kenya na Uganda baada ya kushinda zabuni ya kuwa wenyeji iliyofanyika Septemba mwaka

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga (CCM).

Sanga alihoji Serikali imefikia wapi katika maandalizi ya AFCON, 2027 kwenye ujenzi wa viwanja na Hoteli nchini. Pia alitaka kufahamu mipango ya ujenzi wa viwanja vya mazoezi kwa timu hizo zitakazoshiriki fainali hizo.

Mbunge wa Makete, Festo Sanga.

Akijibu maswali hayo, Mwana FA amesema kwa upande wa Tanzania maandalizi ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu hususani viwanja unaendelea ambapo Serikali imeanza Ujenzi wa Uwanja wa Mpira katika Jiji la Arusha ambao utakua na uwezo wa kubeba watazamaji 30,000.

“Vilevile, katika mwaka wa fedha 2023/24 Serikali inakarabati Uwanja wa Uhuru na Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanya ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Amaan. Sambamba na ujenzi na ukarabati wa viwanja unaoendelea, Serikali ina mpango wa kujenga viwanja katika Jiji la Dodoma na Fumba, Zanzibar

Kuhusu viwanja vya mazoezi, Naibu waziri huyo amesema pamoja na ujenzi wa ujenzi wa viwanja vya mashindano, miji yote itakuwa na viwanja vitano vya mazoezi ambapo vinne ni kwa ajili ya timu na kimoja kwa ajili ya wamuzi.

Related Posts