Taarifa kwa vyombo vya habari

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuanzia Desemba 2023 hadi tarehe 22 Mei 2024 limekuwa na Operesheni kali  maalum  ikihusisha kamisheni mbalimbali za Polisi ikiwemo ile ya kisayansi na kuwezesha kupatikana kwa magari 12 ya wizi ambayo tayari yamekwisha  tambuliwa na wamiliki baada ya uchunguzi pia bajaji 5 zimepatikana.

Katika operation hii amekamatwa  Haruni Selemani @Haruni (34) mkazi wa Yombo Makangarawe, Temeke na wenzake 3.

Watuhumiwa hao walikuwa wakiyaiba magari hayo, kufuta namba za usajili wa gari (Chesess) na kubadilisha plate namba halafu  kuyauza tena yakiwa na kadi za bandia.

Katika hatua nyingine Polisi Dar es Salaam imewakamata watuhumiwa 3 akiwemo Ezekiel  Amani (30) @makundi mkazi wa Buza Kanisani na wenzake 2 kwa kuhujumu miundonu ya shirika la umeme TANESCO.

Watuhumiwa hao wamekamatwa tarehe 15 Mei 2024 eneo la Kisarawe II, Kigamboni wakiwa wanaiba nyaya za umeme zilizokuwa juu kwenye nguzo.


Aidha watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na waya wa umeme wenye urefu wa mita 572 wa 50mm waliokuwa tayari wamekwishaukata, Gloves za kushikia nyanya  za TANESCO  pea moja, mkanda wa kupandia kwenye nguzo na Socket Braker.

Watuhumiwa hao wezi wa nyaya watafikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zao.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na Jeshi halitakuwa na huruma kwani litawashughulikia vikali kwa mifumo ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani

Related Posts