Tanzania mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Uvuvi barani Afrika (AFRICA SMALL SCALE FISHERIES SUMIT 2024)

Katika jitihada za dhati za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha nchi inakuza uchumi wake, kupitia rasilimali ya maji iliyonayo almaarufu kama Uchumi wa Buluu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeandaa mkutano mkubwa wa Uvuvi barani
Afrika (AFRICA SMALL SCALE FISHERIES SUMIT 2024) utak aohusisha mataifa mbalimbali ya Afrika, utakaofanyika Tanzania.

Mkutano huu unalenga  kuleta  chachu ya kubadilishana mawazo, fursa na teknolojia mbalimbali za kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa kwenye utekelezaji wa dhana ya kujenga kesho iliyo bora kwa vijana wetu (BBT), na kufikia malengo makubwa kwenye Uchumi wa Buluu.

Pamoja na mambo mengine, Mutano huo utatumika kama Jukwaa litakolokutanisha wavuvi wetu na wenzao kujadili mafanikio na changamoto zinazowakabili didi ya mustakabali wao.

Vilevile, Mkutano huu utajumuisha maadhimisho ya miaka 10 ya utekelezaji wa Mwongozo wa Uvuvi Mdogo na Muundo wa kisera wa kusimamia Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji barani Afrika, na pia utaangazia fursa zilizopo katika Uchumi wa Buluu.

 ‘Tanzania itakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa mwenyeji wa Mkutano huu,na sababu kubwa ya Tanzania kupata fursa hii ni ongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliiwezesha Wizara yangu kuibuka kinara wa utekelezaji wa Mongozo wa Uvuvi mdogo, na kuwa nchi ya kwanza duniani kuandaa Mpango Mkakati wa kutekeleza Mwongozo huo, na kuifanya Tanzania kung’ara kimataifa, ambapo mwaka jana mwezi Machi, 2023 nilialikwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Italia, kama mgeni rasmi kutoa hotuba kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Uvuvi,ambapo nilito uzoefu wetu wa kuandaa na kutekeleza Mpango Mkakati huo, na pia nilitangaza nia ya Tanzania kuwa mwenyeji kwa mkutano huo mwaka 2024’ Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (mb) 

Related Posts