Highlights on the launch of ‘SIMU MPYA KWENYE
MFUMO WA MILIKI SIMU, LIPA MDOGO MDOGO’ Vodashop Paloma, May 2024
Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom
Tanzania, Bwana. George Lugata amesema
Lengo mojawapo la Vodacom Tanzania PLC ni kuhakikisha
tunaipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, na hili litafikiwa kwa
kuwaletea Watanzania intaneti yenye kasi na ubora wa hali ya juu, lakini pia
hii inatakiwa iende sambamba na vifaa thabiti.
Kama mnavyojua sasa hivi Sisi ni Zaidi ya Mtandao, kwa
maana kwamba huduma na bidhaa zetu zimevuka Kiwango cha kuwa mtandao tu,
tunafanya vitu na kutoa huduma ambazo ni Zaidi ya Mtandao.
Katika muendelezo wa kuhakikisha kila mtanzania
anamiliki SIMUJANJA na anaingia katika ulimwengu wa kidigitali, leo
tunatambulisha kwenu aina nne mpya za simu ambazo mteja wetu wa Vodacom ataweza
kupata katika maduka yetu, kupitia mfumo wetu wa mkopo wa simu(Miliki Simu,
Lipa Mdogo Mdogo).
Lakini pia kupitia menu yetu ya *150*00*44# mteja
ataweza kuangalia aina ya simu ambayo ataweza kukopa na malipo ya awali
atakayotakiwa kulipia ili kuchukua simu kwenye maduka yetu.
Simu ambazo tumeziongeza ni pamoja na Neon Ultra,
Samsung A05, A05s na A15. Mteja ataweza kujipatia:
1.
Neon Ultra kwa kianzio cha TZS, 30,000 na kulipia kila siku TZS
1,000 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani
sms 10.
2.
Samsung
A05 kwa kianzio cha TZS, 45,000 na
kulipia kila siku TZS 1,400 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani
sms 10.
3. Samsung A05s kwa kianzio cha TZS, 55,000 na
kulipia kila siku TZS 1,800 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani
sms 10.
4.
Samsung
A15 kwa kianzio cha TZS, 70,000 na
kulipia kila siku TZS 2,200 nakufurahia 200MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani
sms 10.
Sote tunafahamu kwamba kwa sasa simu Sio anasa, bali
ni kitu cha muhimu sana kuwa nacho, mbali na kuitumia kama chombo cha
mawasiliano lakini mtu anaweza kuitumia kama kitendea kazi.
Nikisema kitendea kazi namaanisha mtu anaweza kufanya
biashara kwa kutumia simu yake ya mkononi, unapokuwa na intaneti madhubuti,
basi unaweza kufanya biashara mtandao (Online business).
Baada ya kusema hayo machache naomba niwashukuru nyote
kwa na niwaombe kutembelea katika maduka yetu Tanzania nchi zima na kujipatia
simu kwa mkopo nafuu na kulipia mdogo mdogo.
George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania
(kushoto)na Edwin Byampanju, Mwakilishi wa Samsung Tanzania wakiwa
katika uzinduzi wa mpango ujulikanao kama ‘Miliki Simu, Lipa Mdogo
Mdogo’ ambao unamwezesha mteja wa Vodacom kulipa kiasi kidogo cha fedha
na kumiliki simu janja huku akiendelea kupunguza deni lake kidogo kidogo
ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, tukio hilo limefanyika Makao Makuu
ya Vodacom Tanzania mnamo tarehe 21 May 2024 jijini Dar es Salaam.