UZINDUZI WA ‘MILIKI SIMU, LIPA MDOGO MDOGO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania (kushoto)na Edwin Byampanju, Mwakilishi wa Samsung Tanzania wakiwa katika uzinduzi wa mpango ujulikanao kama ‘Miliki Simu, Lipa Mdogo Mdogo’ ambao unamwezesha mteja wa Vodacom kulipa kiasi kidogo cha fedha na kumiliki simu janja huku akiendelea kupunguza deni lake kidogo kidogo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, tukio hilo limefanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania mnamo tarehe 21 May 2024 jijini Dar es Salaam.

 

Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Bwana. George Lugata

 

  • Lengo mojawapo la Vodacom Tanzania PLC ni kuhakikisha tunaipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, na hili litafikiwa kwa kuwaletea Watanzania intaneti yenye kasi na ubora wa hali ya juu, lakini pia hii inatakiwa iende sambamba na vifaa thabiti.

 

  • Kama mnavyojua sasa hivi Sisi ni Zaidi ya Mtandao, kwa maana kwamba huduma na bidhaa zetu zimevuka Kiwango cha kuwa mtandao tu, tunafanya vitu na kutoa huduma ambazo ni Zaidi ya Mtandao.

 

  • Katika muendelezo wa kuhakikisha kila mtanzania anamiliki SIMUJANJA na anaingia katika ulimwengu wa kidigitali, leo tunatambulisha kwenu aina nne mpya za simu ambazo mteja wetu wa Vodacom ataweza kupata katika maduka yetu, kupitia mfumo wetu wa mkopo wa simu(Miliki Simu, Lipa Mdogo Mdogo).

 

  • Lakini pia kupitia menu yetu ya *150*00*44# mteja ataweza kuangalia aina ya simu ambayo ataweza kukopa na malipo ya awali atakayotakiwa kulipia ili kuchukua simu kwenye maduka yetu.

 

  • Simu ambazo tumeziongeza ni pamoja na Neon Ultra, Samsung A05, A05s na A15. Mteja ataweza kujipatia:
  1. Neon Ultra kwa kianzio cha TZS, 30,000 na kulipia kila siku TZS 1,000 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani sms 10.
  2. Samsung A05 kwa kianzio cha TZS, 45,000 na kulipia kila siku TZS 1,400 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani sms 10.
  3. Samsung A05s kwa kianzio cha TZS, 55,000 na kulipia kila siku TZS 1,800 nakufurahia 100MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani sms 10.
  4. Samsung A15 kwa kianzio cha TZS, 70,000 na kulipia kila siku TZS 2,200 nakufurahia 200MBs, dakika 10 na jumbe fupi yaani sms 10.

 

  • Sote tunafahamu kwamba kwa sasa simu Sio anasa, bali ni kitu cha muhimu sana kuwa nacho, mbali na kuitumia kama chombo cha mawasiliano lakini mtu anaweza kuitumia kama kitendea kazi.

 

  • Nikisema kitendea kazi namaanisha mtu anaweza kufanya biashara kwa kutumia simu yake ya mkononi, unapokuwa na intaneti madhubuti, basi unaweza kufanya biashara mtandao (Online business).

 

  • Baada ya kusema hayo machache naomba niwashukuru nyote kwa na niwaombe kutembelea katika maduka yetu Tanzania nchi zima na kujipatia simu kwa mkopo nafuu na kulipia mdogo mdogo. 

 

Related Posts