Dc Mkinga awataka watendaji kutumia vizuri matokeo ya sensa kwenye kupanga ujenzi wa miradi kwenye maeneo yao.

Mkuu wa wilaya ya Mkinga Gilbert Kalima amewataka viongozi wa serikali za mitaa,kata,tarafa na wilaya kuhakikisha wanatumia matokeo ya sensa katika kupanga mipango endelevu ya kuwaletea maendelo kwenye maeneo yao.

Kalima ameyasema hayo kwenye mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi,kwa viongozi na watendaji wa wilaya ya Mkinga mkoani na kusema Lengo kuu la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo wa kutafri,kuchambua na kuyatumia matokeo ya sensa katika kupanga,kutekeleza, kufatilia na kutathimii utekelezaji wa sera na mipango ya muda mfupi,muda wa kati na muda mrefu.

“wilaya yetu imekuwa na matukio mengi sana ya ukatili hivyo ni muhimu sana kutumia matokeo ya sensa katika kupiga vita vitendo vya hivyo, hivyo ni wajibu wetu kama viongozi kusimamia kwa pamoja kuisaidia serikali kutokomeza vitendo hivyo ili kuwezesha jamii kuishi kwa amani na utulivu na kuweza kuleta maendeleo kwenye jamii yetu”

Aidha akizungumza kwa niaba ya Mtakwimu mkuu wa serikali Benedict Mugambi ambaye ni afisa takwimu amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa kamati za ulinzi na usalama kutumia matokeo ya sensa ya watu na makazi katika kushauri masuala mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao.

Hata hivyi kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022,halmashauri ya wilaya Mkinga ina jumla ya watu 146,802 ambapo wanaume w ni 73,048 na wanawake 73,754.

Related Posts