Mataifa ya G7 kutathmini mkopo kwa Ukraine – DW – 24.05.2024

Mitazamo ya kimaoni ya maafisa kabla ya mkutano huo wa Stresa, kaskazini mwa Italia yanaonesha kwamba hakutakuwa na ugumu utakayojitokeza kwa msukumo wa Marekani katika utolewaji wa mkopo kwa Ukraine kutokana na mapato ya baadhi ya kiasi cha dola bilioni 300  cha mali za Urusi zilizozuiliwa.

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amesema mkopo unaweza kuwa kiasi cha dola bilioni 50, lakini hakuna kiasi kilichokubaliwa. Awali msaidizi wa Yellen katika mahusiano ya kimataaifa Jay Shambaugh alikiambia kituo cha televisheni cha CNBC kuwa hatarajii mawaziri kujadili masuala ya kiufundi kama vile muundo wa mkopo, nani angesimamia au jinsi kuzuiliwa kwake.

Mtazamo wa Ujerumani katika kuikopesha Ukraine

Ukraine | Uharibifu huko Kharkiv
Polisi anafanya kazi katika eneo la shambulio la anga la Urusi, huko Kharkiv, Ukraine Mei 22, 2024.Picha: Sofiia Gatilova/REUTERS

Nae Christian Lindner ni waziri wa fedha wa Ujerumani  amenukuliwa na akitoa mtazamo kama huo, “Hili ni suala la majadiliano. Masuala mengi ya kisheria na kiufundi bado hayajaeleweka. Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Serikali ya Shirikisho, inachunguza na pia iko tayari kuchukua hatua zaidi ikiwa hayatakuwa na madhara yoyote ya kisheria au athari za kiuchumi. Hili bado haliko wazi kwa sasa kwa sababu mapendekezo bado hayajakamilishwa.”

Mawaziri hao wa G7  Jumamosi wataungana na Waziri wa Fedha wa Ukraine Serhiy Marchenko, ambaye nchi yake inakabiliwa na vita wakipambana kuzuia mashambulizi ya Urusi kaskazini na mashariki, ikiwa ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu uvamizi wa Urusi.

Mapema Jumanne hii, Umoja wa Ulaya ulikamilisha makubaliano yake ya kutumia faida “isiyotarajiwa na isiyo ya kawaida” iliyopatikana kwa kudhibiti mali za Urusi na kutarajia kutoa euro bilioni 15 hadi 20 kwa Ukraine hadi ifikapo mwaka 2027.

Mpango mpya wa ushuru kwa makampuni tajiri duniani

Katika hatua nyingine Waziri wa fedha wa Ufaransa  Bruno Le Maire amesema “amedhamiria” kuendeleza ushuru wa utajiri wa kimataifa, licha ya wasiwasi kutoka kwa Marekani na Ujerumani na mataifa mengine ambayo hayajakamilisha mchakato wa mageuzi ya sera ya utozaji kodi.

Awali Alhamis, Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen, ambaye pia anaudhuria mkutano wa nchi tajiri kiviwanda za kundi la G7, alitoa maoni yake kupinga mpango huo ambao umeungwa mkono na Brazil wakati wa urais wake wa kuongoza kundi la G20.

Soma zaidi:Putin: Hakuna mpango kuukamata mji wa Kharkiv kwa sasa

Yellen alisema anapinga uundwaji huo maalum ambao ungegawanya mapato kati ya nchi kulingana na ushirikia wao katika suala la athari za mabadiliko ya tabia nchi. Baadae Ijumaa hii Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner kuwa Berlin, pia alisema “Ujerumani inatazama vipengele vipya vya ajenda ya kodi ya kimataifa kwa mashaka makubwa”, akitaka kuzingatia kile ambacho tayari wamekifanyia kazi.

Lakini Le Maire anaonesha kuwa maendeleo katika ushuru wa utajiri yanawezekana licha ya upinzani. Takriban nchi 140, ikiwa ni pamoja na Marekani, zimekubaliana kuhusu uuundwaji mpya wa kimataifawa kodi kwa makampuni makubwa zaidi.

Chanzo: RTR/AFP

 

Related Posts