Mungai ashinda uenyekiti Chadema Iringa

Iringa. Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai ameshinda nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Mungai ameshinda nafasi hiyo baada ya kuzoa kura 45 dhidi ya kura 34 ambazo mpinzani wake, Emmanuel Chengule amepata.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo John Mrema amesema kila mgombea alipata haki ya kujieleza na kuchaguliwa.

Katika ngazi ya ukatibu, Leonard Kwirijira ameshindwa kwa kupata kura 46 wakati David Mfugwa amepata kura 35.

Kwa upande wa Bawacha, Susan Mgonokulima amepata kura 15 wakati mshindani wake Hamida Tanda akipata kura 14.

Akizungumza na Mwananchi baada ya kumalizika uchaguzi, Chengula amesema anakubadiliana na matokeo na Mwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki.

“Kama unavyojua tabia za wajumbe ni zile zile za kubadilika badilika, nyingine zimebadilika asubuhi na kama unavyojua tabia za wajumbe ni zilezile zile na waliopatikana tunawaheshimu kama viongozi,” amesema Chengula.

Chengula ambaye ni wakilia msomi amesema msimamo wake ni kuendelea kukupenda chama hicho.

Awali, akishukuru Mungai aliwashukuri wajumbe kwa kumpambania na kumoatia kura hizo.

Related Posts