NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imesema Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wateja wake ambao ni taasisi za Serikali kushindwa kulipa kodi ya pango kiasi cha Sh. 2.1. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo bungeni jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Najma Giga wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo.

Amesema kamati inashauri Serikali kuzisimamia taasisi zinazodaiwa na Shirika hilo kwa kuhakikisha zinatenga bajeti ya kulipa deni hilo.

Awali akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/2025, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema katika mwaka 2023/24, NHC imekusanya Sh. 7.2 bilioni ambapo kiasi cha Sh. 4.1 bilioni ni deni la pango la nyumba, Sh. 2.7 bilioni kutoka kwenye miradi ya ukandarasi na Sh. 400 milioni ni madeni mengineyo ikiwemo ya uuzaji wa nyumba.

“Madeni hayo yamepungua kutoka Sh. 25.7 bilioni Julai, 2023 hadi Sh. 18.5 bilioni Mei, 2024 sawa na asilimia 28,”a amesema.

Hata hivyo, amesema Shirika hilo bado linakabiliwa na changamoto ya wadaiwa sugu wa kodi ya pango; miradi ya ukandarasi na wanunuzi wa nyumba kutokukamilisha malipo yao kwa wakati.

Amesema shirika limeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba na wapangaji ili kuwaruhusu kulipa madeni yao kwa awamu na kuvunja mikataba ya upangaji kwa wapangaji waliokaidi kulipa madeni yao na kuwaondoa kwenye nyumba na kukamata mali zao kwa ajili ya kuuza ili kufidia madeni yao.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.

“Pia kuwatangaza wadaiwa sugu katika vyombo vya habari; kuhakikisha kuwa, kila mpangaji mpya anayepangishwa analipa amana ya pango ya miezi mitatu (security deposit); na kuingia makubaliano na Credit Information Reference Bureau ili kusajili majina ya wadaiwa sugu na kuwanyima fursa ya kupata mikopo katika taasisi za fedha.

“Kuingia mikataba na wapangaji ili kuwaruhusu kulipa madeni yao kwa awamu; Kuvunja mikataba ya upangaji kwa wapangaji waliokaidi kulipa madeni yao na kuwaondoa kwenye nyumba na kukamata mali zao kwa ajili ya kuuza ili kufidia madeni yao; Kuwatangaza wadaiwa sugu katika vyombo vya habari; Kuhakikisha kuwa, kila mpangaji mpya anayepangishwa analipa amana ya pango ya miezi mitatu (security deposit); na Kuingia makubaliano na Credit Information Reference Bureau ili kusajili majina ya wadaiwa sugu na kuwanyima fursa ya kupata mikopo katika taasisi za fedha,” amesema.

Aidha, ametoa wito kwa wapangaji kulipa ankara zao kwa wakati na wadaiwa wote kulipa madeni yao mapema kabla hatua zaidi hazijachukuliwa kwa ukiukaji wa mikataba.

Related Posts