Rais wa CAF amewasili Unguja Zanzibar kushuhudia fainali za African Schools Football

Rais was Shirikisho la soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe amewasili Unguja Zanzibar leo kwa ajili ya kutazama fainali za African Schools Football.

Motsepe baada ya kuwasili nchini aliongea na Waandishi wa Habari na kuongea mambo mbalimbali ikiwemo utata wa goli la Yanga dhidi ya Mamelod Sundowns kule Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali uliyochezwa April 5 2024.

“Kama Rais wa CAF napenda nchi zote 54 Wanachama wa CAF na Vilabu vyote, tulipokutana na Rais Wallace (Rais TFF Wallace Karia) baada ya mechi ya Yanga na Mamelod nilimwambia kuwa nafikiri lilikuwa goli lakini Rais wa CAF hatakiwi kutoa maoni yake lakini tunatakiwa kuheshimu kanuni na sheria za soka na VAR” >>>

Related Posts