Hatua hii imepingwa vikali na Waserbia wanaohofia kuwa itawafanya wote kuwa waungaji mkono wa mauaji ya halaiki. Kura hiyo katika Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa lenye jumla ya wanachama 193, imepita kwa kuungwa mkono na mataifa 84 dhidi ya 19 yaliopinga, huku mengine 68 yakijizuwia kupiga kura.
Soma piaUholanzi yaiomba radhi Srebrenica kwa mauaji:
Azimio hilo linaitaja Julai 11 kama siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya mauaji ya halaiku ya Srebrenica, itakayoadhimishwa kila mwaka kuanzia miezi miwili ijayo.
Azimio hilo lililofadhiliwa na Ujerumani na Rwanda haliwataji moja kwa moja Waserbia kama wahusika wakuu wa mauaji hayo lakini lilipingwa vikali rais wa Bosniaya Serbia Milorad Dodik, na rais wa Serbia Aleksandar Vucic, aliejizungushia bendera ya Serbia akiwa ameketi barazani wakati wa kura.