Makamu Mwenyekiti wa CCM BARA COMRADE Abdulrahman Kinana ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoa mafunzo ya mara kwa mara yanayolenga kujenga uwezo kwa Viongozi na Watendaji Wanawake nchini.
Comrade Kinana ametoa pongezi hizo leo Mei 25, 2024 akifungua mafunzo ya Wanawake wanasiasa yaliyoandaliwa na UWT Jijini Dodoma.
Washiriki wa mafunzo hayo ni Wabunge wanawake wa CCM wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Watendaji wanawake wa CCM kutoka jumuiya ya wazazi,Wenyeviti wa CCM Wanawake wa Mikoa na Wilaya.