Kwanini kilimo na afya ya udongo ni tatizo Afrika?

Leo ikiwa ni siku ya Afrika,tujadili hili la kilimo na usalama wa udongo Afrika, athari zake bila kusahau utatuzi wake. Lugha ya sokoni kati ya wauzaji na wanunuzi katika masoko ya kawaida ya watu wa hali ya chini wanaoishi chini ya dola mbili kwa siku barani Afrika sasa hawaongei lugha moja katika maelewano ya mteja na mnunuzi. Wauzaji wanasikika wakisema siwezi kukupunguzia bei ya kitunguu kwa sababu hata huko ninakovifuata ni adimu,huku wanunuzi wakisema jamani mbona bei ni tofauti na ulivyokuwa unaniuzia zamani?lakini chanzo ni Mafuriko na Ukame,kwani uzalishaji wake umeshuka kutokana na athari hizo.

Ufuatiliaji wa MubaliMedia katika baadhi ya masoko nchini Tanzania ulibaini mabadiliko makubwa ya bei za vitunguu,mfano katika masoko yaliyo mengi Vitunguu Swaumu vimepanda na kufikia shilingi 25,000 kwa kilo moja,ya sokoni imekuwa ya malalamiko zaidi kati ya mteja na muuzaji, mvua kubwa zilizonyesha zikijumuishwa kwenye lawama hizo.

 

Hali inayopelekea wimbi la hali ngumu ya kiuchumi, matumizi yanazidi kipato na ‘mikopo kausha damu’ inachukua mkondo wake.

Athari zinaelekezwa kwa mtu mmoja mmoja kuanzia kwenye afya ya akili, kwa sababu kwa sasa shilingi 5,000 kwa kilo moja ya vitunguu maji,nyanya ndoo ndogo kabisa shilingi 7,000 ni gharama zinazosababisha msongo wa mawazo kwa watumiaji wa kipato cha chini.

Kupanda huku kwa bei kunakuja huku vipato vya watu vikiwa vimeathirika pia kutokana na majanga hayo ambayo kwa namna moja ama nyingine yameyumbisha hadi uchumi wa nchi za Afrika.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat mapema mwezi huu katika Mkutano Mkuu wa azimio la Nairobi kuhusu Mbolea na Afya ya udongo Afrika,alikaririwa akisema kuwa Mafuriko na Ukame unaoushuhudiwa kwa sasa barani Afrika, unatoa angalizo dhidi ya kupungua kwa uzalishaji wa chakula katika sekta ya kilimo jambo linaloweza kuongeza hali mbaya kwa Afrika.

 

Changamoto za uhaba wa chakula, lishe duni, na mabadiliko ya tabianchi vinaendelea kuwepo na hatua za haraka zikihitajika,aliongeza Mousa Faki Mahamat.

Related Posts