LALJI FOUNDATION WAENDESHA KAMBI YA MAALUM YA MATIBABU YA AFYA BURE KASULU

Taasisi isiyo ya kiserikali ya LALJI FOUNDATION kwa kushirikiana na GAME FRONTIERS OF TZ, KIGOMA HILLTOP HOTEL na Hospitali ya Wilaya ya Kasulu wameendesha kambi maalum ya matibabu ya afya bure kwa wakazi wa Kasulu kuanzia mei 22 mpaka mei 25, 2024.

Katika kambi hiyo iliyofanyika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu wagonjwa zaidi ya 2500 wanakadiriwa kujitokeza ambapo walipatiwa huduma mbalimbali za matibabu kama vile Matibabu ya Macho Upasuaji Kupima Shinikizo la Damu

Kupima kisukari I Magonjwa ya Akina Mama na Watoto Upasuaji wa Mifupa huku watu 200 wakifanyiwa Upasuaji wa magonjwa ya macho.

Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa kambi hiyo Mwenyekiti wa taasisi ya LALJI FOUNDATION ndugu Imtiaz Lalji na Mkurugenzi wa Game Frontiers na Kigoma Hilltop Hotel ndugu MohamedTaki Lalji wamebainisha kuwa muitikio mkubwa kwa wananchi wa Kasulu kujitokeza katika kambi hiyo kunawapa ari ya kuendelea na zoezi hilo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi walipongeza waandaaji wa kambi hiyo ambapo imewasaidia kujua afya zao hivyo kuchukua hatua ikiwemo suala la kuzingatia kanuni za kufuata pamoja na ushahuri wa kitabibu.

Related Posts